Friday, August 7, 2015

UEFA WAMALIZA UBISHI, MAN UTD YAPELEKWA UBELGIJI
By j.twice
Muda mchache uliopita shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limekamilisha upangani wa michezo ya mtoano ya ligi ya mabingwa barani humo.

Man Utd ambayo ni moja ya klabu zilizopo kwenye mchakato huo imeangukia mikononi mwa FC Club Bruge ya nchini Ubelgiji.

Man Utd wataanzia nyumbani Old Trafford na kisha watamalizia mchezo wa mkondo wa pili ugenini

Michezo mingine iliyopangwa katika zoezi hilo.

Lazio v Bayer Leverkusen

Manchester United v Club Brugge

Sporing v CSKA Moscow

Rapid Vienna v Shakhtar Donetsk

Valencia v Monaco

Astana v Apoel

Skenderbeu v Dinamo Zagreb

Basel v Maccabi Tel Aviv

BATE v Partizan

Celtic v Malmo

Michezo ya hatua ya mtoano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya imepangwa kuchezwa August 18/19 na ile ya mkondo wa pili itachezwa August 25/26.

Wednesday, July 22, 2015

MEEK MILL ASEMA DRAKE, HAJUI KUANDIKA MASHAIRI
Created by j.twice
Saa kadhaa zilizopita rapa Meek Mill ameporomosha maneno yanayoonekana kumchafua rapa mwenzake Drake na kudai kuwa rapa huyo hawezi kuandika verses zake na mara nyingi huwa amekuwa akiandikiwa.

Kwa kutumia akaunti ya twita Meek Mill ameandika maneno yaliyomaanisha kwamba, Drake hawezi kuandika na mara nyingi amekuwa akiandikiwa.

“Hata mimi niliwahi kumuandikia katika moja ya albamu yake, lakini jamaa ameshindwa kuonyesha shukrani, ningejua nisingefanya hivyo”, aliandika Meek Mill.

Meek Mill aliendelea kwa kusema kwamba marapa wengi wanalijua hilo hata Lil Wayne na Nick Minaj ukiwauliza wataongea ukweli.

Naye Rick Ross alitoa maoni kwenye twita ya Meek Mill na kuonyesha kukubaliana naye kwamba ni kweli Drake amekuwa akiandikiwa nyimbo zake.

“ @MeekMill speaking facts!!!! Luv mynigga 4L #Empire ”, aliandika Rick Ross.

Pia Meek Mill aliwapongeza Kendrick Lamar na J. Kole kwamba wawili hao wanajua sana kufanya muziki sema bado hawapo kwenye laini nzuri.

Bado Drake hajajibu chochote kuhusu hilo, swalui lilobaki je ni nini atakachokijibu baada ya tuhuma hizo toka kwa Meek Mill.

Monday, July 20, 2015

wanaoiwakilisha Tanzania kwenye Tuzo za AFRIMMA 2015 wako saba, list ya wote ninayo hapa.. By j.twice


Najua itakuwa furaha kubwa kwa kila mtu ambae anatoa love na suppoort ya kutosha kwa wasanii wa TZ, inapendeza kuona majina ya mastaa wetu wanaofanya muziki wanazidi kufahamika nje ya mipaka yetu.

MTV MAMA 2015 imeshafanyika Durban South Africa ambapo TZ ilikuwa ikiwakilishwa na mastaa wawili tu, Diamond Platnumz na Vanessa Mdee… lakini kabla mambo hayajapoa nakutana na hii, kiukweli kwetu ni GOOD NEWS… Tuzo za AFRIMMA zitafanyika Dallas Marekani October 2015 na hapa tayari imenifikia hii list ya mastaa waliochaguliwa kuwania Tuzo hizo, ni furaha kubwa kuona idadi ya wawakilishi wa Tanzania na East Africa safari hii wamekuwa wengi zaidi.

Best Male West Africa

Davido (Nigeria)

Serge Beynaud (Ivory Coast)

Wizkid (Nigeria)

Sarkodie (Ghana)

Flavour (Nigeria)

Carlou D (Senegal)

Olamide (Nigeria)

Stonebwoy (Ghana)

Best Traditional Artist

Flavour (Nigeria)

Kwabena Kwabena (Ghana)

Dobet Gnahore (Ivory Coast)

Ladysmith Black Mambazo (South Africa)

Mrisho Mpoto (Tanzania)

Soweto Gospel Choir (South Africa)

Tunakie (Namibia

Best Female West Africa

Yemi Alade (Nigeria)

Wiyaala (Ghana)

Tiwa Savage (Nigeria)

Viviane Child (Senegal)

Teeyah (Ivory Coast)

Becca (Ghana)

Almok (Togo)

Efya (Ghana)

Best Newcomer

Kiss Daniel (Nigeria)

Pappy Kojo (Ghana)

Korede Bello (Nigeria)

Lil Kesh (Nigeria)

Mz Vee (Ghana)

Fabregas (Congo)

Ommy Dimpoz (Tanzania)

Bebe Phillip (Ivory Coast)

Best Male East Africa

Eddy Kenzo (Uganda)

Jaguar (Kenya)

Diamond Platnumz (Tanzania)

Bebe Cool (Uganda)

Jackie Gosse (Ethiopia)

Ali Kiba (Tanzania)

Dynamq (South Sudan)

Best Video Director

Moe Musa (Nigeria)

Godfather (South Africa)

Clarence Peters (Nigeria)

Patrick Ellis (Nigeria)

Klasszik & JKP Studio (Angola)

Justin Campos (South Africa)

Ogopa Djs (Kenya)

Phamous Films (Ghana)

Best Female East Africa

Khadija Kopa (Tanzania)

Aster Aweke (Ethiopia)

Victoria Kimani (Kenya)

Vanessa Mdee (Tanzania)

Juliana Kanyamozi (Uganda)

STL (Kenya)

Irene Ntale (Uganda)

Best DJ Africa

Dj Jimmy Jatt (Nigeria)

Dj Exclusive (Nigeria)

Dj Cndo (South Africa)

Dj Black (Ghana)

Dj Creme de la Creme (Kenya)

DJ Shiru (Uganda)

Dj Joe Mfalme (Kenya)

Best Male Central Africa

Fally Ipupa (DR Congo)

Yuri Da Cunha (Angola)

Fabregas (Congo)

Nelson Freitas (Cape Verde)

Ferra Golla (Congo)

Corean Du (Angola)

Jovi (Cameroon)

Youssoupha (DRC)

Best African DJ – USA

DJ Shinski (Kenya)

DJ Ebou (Gambia)

DJ Ecool (Nigeria)

DJ Ronnie (Ghana)

DJ Dee Money (NG/US)

DJ Ronnie (GH/US)

Dj Amin (Ethiopia)

Dj Dozzy Ross (Nigeria)

Best Female Central Africa

Arielle T (Gabon)

Coco Argentee (Cameroon)

Betty Akna (Equitorial Guinea)

Lady Ponce (Cameroon)

Yola Semedo (Angola)

Laurette Le Pearle (DRC)

Mani Bella (Cameroon)

AFRIMMA Video of the Year

R2bees – Lobi (Ghana)

Wizkid Ojuelegba (Nigeria)

Flavour – Gollibe (Nigeria)

Diamond ft Flavour – Nana (Tanzania)

Tiwa Savage – My Darlling (Nigeria)

Bebe Cool – Love You Everyday (Uganda)

Juliana Kanyomozi – Woman (Uganda)

AKA – Congratulate (South Africa)

Best Male Southern Africa

AKA (South Africa)

Zeus (Botswana)

Cassper Noyvest (South Africa)

Slap Dee (Zambia)

Stunner (Zimbabwe)

Tha Dogg (Namibia)

Donald (South Africa)

Vee (Botswana)

Music Producer of the year

Shizzi (Nigeria)

Don Jazzy (Nigeria)

Killbeatz (Ghana)

Oskido (South Africa)

Nash Wonder (Uganda)

Sheddy Klever (Tanzania)

Legendary Beatz (Nigeria)

Dj Breezy (Ghana)

Best Female Southern Africa

Bucie (South Africa)

Toya De Lazy (South Africa)

Ice Queen Cleo (Zambia)

Busiwa (South Africa)

Punah Gabasiane (Botswana)

Lizha James (Mozambique)

Samantha Mogwe (Botswana)

Best Dance Group

CEO Dancers

Unique Silver Dancers

Level 5

Imagneto Dance Company

D3 Dancers

Best African Group

square (Nigeria)

Bana C4 (Congo)

Toofan (Togo)

Sauti Sol (Kenya)

B4 (Angola)

Black Motion (South Africa)

R2bees (Ghana)

Magic System (Ivory Coast)

Best Rap Act

Sarkodie (Ghana)

AKA (South Africa)

Olamide (Nigeria)

NGA (Angola)

Octopizzo (Kenya)

Phyno (Nigeria)

Cassper Noyvest (South Africa)

M.I (Nigeria)



Crossing Boundaries with Music

Fuse ODG (Ghana)

Wale (Nigeria)

Knaan (Somalia)

Nneka (Nigeria)

STL (Kenya)

Asa (Nigeria)

Jidenna (Nigeria)

Tinnie Tempah (Nigeria)

Best Collaboration

Harrysong, K Cee & Iyanya – Feel it

J Martins ft Koffi Olamide – Dance for Me

Serge Beynaud ft Eddy Kenzo – Lopangwe

AKA ft Burna Boy, Da L.E.S & J.R – All Eyes on Me

Toofan ft Dj Arafat – Apero

Stanley Enow ft Sarkodie – Njama Njama Cow Remix

P Square ft Don Jazzy – Collabo

Diamond ft Flavour – Nana



Best Dancehall Artist

Stonebwoy (Ghana)

Timaya (Nigeria)

MC Norman (Uganda)

Wax Dey (Cameroon)

Dr Jose Chameleon (Uganda)

Shatta Wale (Ghana)

Patoranking (Nigeria)

Buffalo Soldier (Zimbabwe)



Song of the Year

Wizkid – Ojuelegba (Nigeria)

Korede Bello – Godwin (Nigeria)

Lil Kesh ft Olamide, Davido – Shoki (Nigeria)

Stonebwoy ft Sarkodie – Baafira (Ghana)

Roberto – Amarula (Zambia)

Diamond Platnumz – Ntampata Wapi (Tanzania)

Sauti Sol – Sura Yako (Kenya)

Cassper Nyovest – Doc Shabaleza (South Africa)



Best Dance in a Video

Lil Kesh ft Olamide, Davido – Shoki (Nigeria)

Toofan – Orobo (Togo)

Sauti Sol – Lipala (Kenya)

Fabregas – Mascara (Congo)

Diamond and Flavour – Nana (Tanzania and Nigeria)

Os DeTroia – Bela (Angola)

Serge Beynaud – Okeninkpin (Ivory Coast)

Olamide – Shakiti Bobo (Nigeria)



Artist of the Year

Flavour (Nigeria)

Davido (Nigeria)

Diamond Platnumz (Tanzania)

Sarkodie (Ghana)

Cassper Noyvest (South Africa)

Fally Ipupa (Congo)

Eddy Kenzo (Uganda)

Wizkid (Nigeria)

Yemi Alade (Nigeria)

Bucie (South Africa)



Best Gospel Artist

Sammy Okposo (Nigeria)

Nikki Laoye (Nigeria)

Soweto Gospel Choir (South Africa)

Uche Agu (Nigeria)

No Tribe (Ghana)

Icha Kavons (Congo)

Ntokozo Mbambo (South Africa)

Willy Paul (Kenya)



AFRIMMA Inspirational Song

Bracket ft Diamond & Tiwa Savage – Alive (Nigeria & Tanzania)

Juliana Kanyomozi – Woman (Uganda)

Sarkodie ft Castro – Adonai (Ghana)

Jose Chameleon – Bwerere (Uganda)

Psquare ft Dave Scott – Bring it On (Nigeria)

Eddy Kenzo – Be Happy (Uganda)

Kwenye list yote nimeona majina haya ya mastaa wa Tanzania >>> Mrisho Mpoto, Ommy Dimpoz, Ali Kiba, Khadija Kopa, Vanessa Mdee, Diamond Platnumz na Producer Sheddy Clever.

Unaweza kuanza kupiga kura kwa mtu wako kuanzia sasahivi mtu wangu, rahisi kabisa yani.. Bonyeza link hii hapa unaingia moja kwa moja >>>> Nominees 2015 | – Afrimma
BAADA YA KUSUBIRIWA KWA MDA MREFUU SASA KWA HEWAA DONALD KUTOKA SOUTH  AFRICA  FT DIAMOND TOKA TZ TANZANII NGOMA WANGU
SHILOLE NA NUH MZIWANDA WAMEMWAGANA? By j.twice
Tangu juzi kumekuwa kukionekana post za sintofahamu za wapenzi wawili Instagram, “stars” wa Bongo flava Nuh Mziwanda na Shilole.
Post hizo zinaonekana kama wapenzi hawa wametofautiana, na kila mmoja amekuwa akitoa udhaifu ama “makavu” mwenzie.

Taarifa hizo zimeonekana kuwachanganya followers na fans wao Instagram, wengine wakidai wanatafuta “Kick” kwa sababu kuna “mkwaju” mpya wameundaa pamoja.

Zitazame post zao hapo chini then tuachie maoni yako mdau.

“Kidume unataka raha tu ‘pesa hauna ‘na bado siunaleta ujanja kwa mtoto wa igunga ‘mjini hapa ‘halafu sina habari ‘wacha niwe busy na kazi zangu tu’mapenzi yashanishinda mie.nawapenda sana mashabiki wangu! Manopenda mitelemko kazi mnayo kupandisha vitonga hamtaki mtanyoookaa na kama ulikuwa unatembelea Kik yangu basi katafute snare
Mwanaume hata umfanyie nini haridhik lol! Pamoja na kukubali shida zake zote lakin mh! Nimejitahid nimehangaika’ila sasa kama gari limewaka’aka babu weeee kanikuta na maisha yangu wacha niendelee na maisha yangu’Mimi na yeye baaaaaaasi #GaNdALaNdiZ” amendika Shilole.

“Mwanaume wa kweli ukaa kimya’sibishani na upumbavu’mwanamke asieridhika na kujua kua kathaminiwa mpaka tatoo kachorwa’na kuvumilia mambo yote alionifanyia ya kuniaibisha mbele ya mashabiki zangu’familia na’wasanii wenzangu na wadau’anaanza kunitukana mitandaoni for whaaaat!!! Mxeeeeew’mimi bado kijana na nna time ya kupata maisha yangu na mtu atakae thamini moyo wangu ‘nawaachia wanaume wenzangu na nyie mjaribu zari ‘mimi nacheka tu #AsHaNgeDerE” haya ameyaandika Nuh.
Msanii wa Nigeria apata dili kwenye lebel ya The Game. By J.twicee



Rapa kutoka Marekani The Game amempa mkataba wa kurekodi msanii kutoka Nigeria ‘Terry G’ kupitia lebel yake ya Black Wall Street Records.

Mpango wa Terry G kupata dili na The Game umefanikishwa na Suni Osorun, Mnigeria mwenye kampuni ya burudani iliyopo Marekani.

Black Wall Street Records ni lebel ya The Game aliyoanzisha na kaka yake ‘Big Fase 100′ Taylor III na Suni Osorun ‘Big Suni’.

 T-Pain naye katusogezea mix tofauti ya Classic Man ndani ya; Classic Man (TMix) – (Video) By j.twice

Wimbo ambao unafanya vizuri kwenye chati za muziki kwa wiki ya pili sasa ni Classic Man remix ya Jidenna aliyomshirikisha HipHop superstaa Kendrick Lamar.

Good news kwako mtu wangu ni kwamba wimbo unazidi kupokelewa vizuri na watu, na msanii wa Pop Crunck nchini Marekani T-pain naye kaweka flava yake kwenye wimbo huo akiwa amewashirikisha wasaani wengine kama Vantrease na Young Cash.

Nimekusogezea video ya mix hiyo hapa

Man U yasema haitaongeza mshambuliaji......kwa sasa......by presenter wako j.twice

Kocha Mkuu wa Manchester United Louis Van Gaal
Kocha mkuu wa Manchester United Louis Van Gaal ametamba kuwa hatanunua mshambuliaji mwingine kwani alio nao kwa sasa wanatosha wakiongozwa na Wayne Rooney.
Pamoja na Wayne Rooney washambuliaji wengine waliobaki ni Javier Hernandes Chicharito, na James Wilson baada ya mshambuliaji mpachika magoli Robin Van Persie kujiunga na Fenerbahce ya Uturuki hivi karibuni na Radamel Falcao mkopo wake kumalizika.
Van Gaal anatarajia kumtumia Rooney kama mshambuliaji pekee pale mbele ambapo atasaidiwa na Mephis Depay aliyesajiliwa wakati wa majira ya joto kutoka PSV Eindhovenya Uholanzi.
Van Gaal anatamba kuwa Depay anaweza kuwa mshambuliaji wa katikati tofauti na alivyokuwa akitumika wakati alipokuwa PSV.

Sunday, July 19, 2015


Casilla achukua nafasi ya Casillas R Madrid.....by j.twiceee


Kiko Casilla
Real Madrid imemsajili kipa wa Espanyol Kiko Casilla kwa pauni milioni 4.2.
Real ilisalia na haki za asilimia 50 za umiliki wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 wakati alipoondoka kujiunga na Espanyol mwaka 2007.
Casilla ambaye ameandikisha sahihi ya miaka 5,atatoa ushindani mkubwa kwa kipa Keylor Navas na Fernando Pecheco.
Real ambayo ilimuuza kipa wa mda mrefu Iker Casillas katika kilabu ya Porto mwezi huu,pia wanamwinda kipa wa Manchester United David De Gea.
Diamond alivyopokelewa Airport Dar baada ya kurudi na Tuzo ya MTV. By j.twice picha na Millard ayo


Mwimbaji staa wa bongofleva Diamond Platnumz July 18 2015 alitangazwa mshindi wa tuzo moja ya MTV MAMA 2015 Category ya Best Live Act ambapo baada ya kuichukua hajaichelewesha, karudi nyumbani Tanzania na haya ndio mapokezi yenyewe kwenye uwanja wa ndege Dar es salaam.

Kabla hajatua uwanja wa ndege tayari kulikuwa na kundi kubwa la watu waliofurika wakiimba muda wote na kushangilia kwenye uwanja huo wa ndege wa Julius Nyerere International Airport kama hivi inavyoonekana kwenye picha.


https://www.youtube.com/watch?v=Tl3paLVzvE0........malalamiko ya Jokate, anasema hii post Ya Diamond Platnumz imemdhalilisha, Video iko hapa. By j.twice



Baada ya kushinda tuzo ya Best Act kwenye tuzo za Mama [Mtv AFrika Music Awards] Msanii wa bongo fleva Diamond Platnumz aliweka picha mbili kuwashukuru mashabiki wake na video moja ikimuonyesha aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Jokate akicheza na kufurahia wimbo wake.

Post hio imechukuliwa kama kumdhalilisha Jokate sababu ya Ukaribu wake na hasimu wa Diamond Platnumz ambaye ni Ali Kiba. Haya maneno ya Jokate baada ya video hiyo kuonekana mtandaoni.




Saturday, July 18, 2015

LVG ADOKEZA-CHICHA KUBAKI OLD TRAFFORD, STRAIKA MWINGINE KUTINGA
By .j.twice




Louis van Gaal amekiri Javier Hernandez 'Chicharito' atapata nafasi nyingine ya kupigania nafasi yake kwenye Kikosi cha Manchester United akiungana na Timu hiyo hapo Julai 25 huko Ziarani Marekani.
Chicharito, ambae aliifungia Man United Bao 59 katika Mechi154, alipelekwa kwa Mkopo huko Real Madrid Msimu uliopita baada Van Gaal kuamua atakuwa nyuma ya Wayne Rooney, Robin van Persie na Radamel Falcao katika kupewa namba.
Lakini, baada ya Man United kuifunga Club America 1-0 mapema Leo, Van Gaal aliulizwa hatima ya Chicharito na kueleza: "Chicharito anakuja Julai 25. Ana nafasi ya kudhihirisha uwezo wake hasa baada ya Falcao na Van Persie kuondoka, hivyo nafasi yake kubwa."
Hivi sasa Man United imebakiwa na Mastraika Wawili tu wanaotambulika ambao ni Kepteni Wayne Rooney na James Wilson na alipoulizwa kuhusu upungufu huo, Van Gaal alijibu: "Hapana tunae Rooney anaweza kucheza kama Straika mkuu. Wanahabari wote Msimu uliopita waliandika anapaswa kucheza hapo na mimi nawasikiliza. Na tunae Chicharito, na labda Wilson, na pengine kwa kushangaza..mpya., huu ni mchakato. Sina wasiwasi na nafasi hiyo."Na hapa nimekusogezea bao la ushindi la united vs club america
2015, wako hapa wote 17 akiwemo na Diamond Platnumz By j.twice
Yako majina mawili yaliyoiwakilisha Tanzania kwenye Category 13 za MTV Africa Music Awards 2015, Diamond Platnumz na Vanessa Mdee ‘Vee Money’… kura zimepigwa na leo ndio ilikuwa fainali yenyewe ndani ya Durban South Africa ukumbi wa Durban International Convention Centre.

Tanzania imetoka kifua mbele pia kwa mara nyingine, Daimond Platnumz kafanikiwa kupata ushindi wa Tuzo ya Best Live Act, ambapo alikuwa katika Category tatu tofauti na Vee Money alikuwa kwenye Category moja.

List ya Washindi wote hii hapa..

Best Female:

Yemi Alade (Nigeria) >>> Mshindi.

Bucie (South Africa)

Busiswa (South Africa)

Seyi Shay (Nigeria)

Vanessa Mdee (Tanzania)

Best Male:

Davido (Nigeria) >>> Mshindi

AKA (South Africa)

Diamond (Tanzania)

Sarkodie (Ghana)

Wizkid (Nigeria)

Best Group:

P Square (Nigeria) >>> Washindi.

B4 (Angola)

Beatenberg (South Africa)

Black Motion (South Africa)

Sauti Sol (Kenya)

Best New Act Transformed by Absolut:

Patoranking (Nigeria) >>> Mshindi.

Anna Joyce (Angola)

Cassper Nyovest (South Africa)

Duncan (South Africa)

Stonebwoy (Ghana)

Best Hip Hop:

Cassper Nyovest (South Africa) >>> Mshindi.

K.O. (South Africa)

Phyno (Nigeria)

Olamide (Nigeria)

Youssoupha (DRC)

Best Collaboration:

AKA, Burna Boy, Da LES & JR: “All Eyes On Me” (South Africa/ Nigeria) >>> Washindi.

Davido featuring Uhuru & DJ Buckz: “The Sound” (Nigeria/SA)

Diamond & Iyanya: “Bum Bum” (Kenya/Nigeria)

Toofan & DJ Arafat: “Apero Remix” (Togo/Ivory Coast)

Stanley Enow & Sarkodie: “Njama Njama Cow Remix” (Cameroon/Ghana)

Song of the Year:

Mavins: “Dorobucci” (Nigeria)>>> Washindi.

Cassper Nyovest: “Doc Shebeleza” (South Africa)

Euphonik featuring Mpumi: “Busa” (South Africa)

DJ Fisherman & NaakMusiQ featuring DJ Tira, Danger & Dream Team: “Call Out” (South Africa)

K.O featuring Kid X: “Caracara” (South Africa)

Lil Kesh Featuring Olamide & Davido: “Shoki Remix” (Nigeria)

Sauti Sol: “Sura Yako” (Kenya)

Toofan: “Gweta” (Togo)

Wizkid: “Show You The Money” (Nigeria)

Yemi Alade: “Johnny” (Nigeria)

Best Live:

Diamond Platnumz (Tanzania) >>> Mshindi.

Big Nuz (South Africa)

Flavour (Nigeria)

Mi Casa (South Africa)

Toofan (Togo)

Video of the Year:

“Nafukwa” – Riky Rick; Director: Adriaan Louw >>> Mshindi.

“Crazy” – Seyi Shay Featuring Wizkid; Director: Meji Alabi

“Doors” – Prime Circle; Director: Ryan Kruger

“Love You Everyday” – Bebe Cool; Director: Clarence Peters

“The Sound” – Davido Featuring Uhuru & DJ Buckz; Director: Sesan

Best Pop & Alternative:

Jeremy Loops (South Africa) >>> Mshindi.

Fuse ODG (Ghana)

Jimmy Nevis (South Africa)

Nneka (Nigeria)

Prime Circle (South Africa)

Best Francophone:

DJ Arafat (Ivory Coast) >>> Mshindi.

Jovi (Cameroon)

Laurette Le Pearle (DRC)

Tour 2 Garde (Ivory Coast)

Toofan (Togo)

Best Lusophone:

Ary (Angola) >>> Mshindi

B4 (Angola)

Nelson Freitas (Cape Verde)

NGA (Angola)

Yuri Da Cunha (Angola)

Personality of the Year:

Trevor Noah (South Africa) >>> Mshindi.

Basketmouth (Nigeria)

Bonang Matheba (South Africa)

OC Ukeje (Nigeria)

Yaya Toure (Ivory Coast)

MAMA Evolution (Category mpya): D’Banj (Nigeria) >>>> Mshindi.

Best International: Nicki Minaj (Mshindi)

Artist of the Decade: P Square (Washindi)

MTV Base Leadership Award: Saran Kaba Jones & S’Bu Mavundla (Washindi)

Thursday, July 16, 2015

Mambo ni haya Man United, Victor Valdes na Kocha Louis Van Gaal hakuna amani kati yao… By j.twice


Ndani ya masaa 72 tu mahusiano mazuri kati ya golikipa wa Manchester United Victor Valdes na kocha wa timu hiyo Louis Van Gaal yamevunjika, tofauti kati yao ilianza wakati Valdes alipogoma kucheza kikosi cha wachezaji wa akiba.



Maswali yalianza kutawala baada ya Valdes kuenguliwa na David de Gea kujumuishwa kikosini licha ya kuhusishwa pia na story kwamba ana mpango wa kuihama klabu hiyo, katika kikosi kilichosafiri na timu kwenda Marekani kwa maandalizi ya msimu mpya.

Valdes ameachwa na timu na wengi walianza kudhani labda kaachwa sababu ya majeruhi kabla ya Van Gaal kufichua ukweli katika kikao na waandish wa habari jumatano hii Marekani.



Lakini sasa majibu kamili ya nini kimetokea kati ya wawili hao kimejulikana, Van Gaal amemuacha Valdes kwa sababu hataki kufuata falsafa zake hivyo ni mtovu wa nidhamu na hana nafasi katika kikosi chake.

“hafuati falsafa zangu, hivyo hakuna nafasi ya mtu kama huyo”>>> Van Gaal

Van Gaal anamtuhumu Valdes kwa utovu wa nidhamu baada ya kukataa kucheza mechi na kikosi cha wachezaji wa akiba akiba msimu uliopita. Kufuatia mvutano huo Valdes kuna uwezekano mkubwa wa kutoendelea kuvaa jezi ya Manchester United msimu ujao.

Valdes alijiunga na Man United january 2015 kama mchezaji huru akiwa amemaliza mkataba wake na klabu  ya FC Barcelona.
 Chelsea nao wametambulisha jezi zao watakazotumia msimu huu By j.twice

Tukiwa tunasubiri kuanza kwa Ligi Kuu Uingereza msimu ujao vilabu kadhaa vimekuwa vikitangaza jezi za mechi za nyumbani na ugenini… Mara nyingi jezi zao huwa hazibadiliki rangi kinachobadilika ni muundo tu wa jezi na wakati mwingine nembo ya mdhamini kutegemeana na Mkataba ambao Klabu wanao.

Sababu mojwapo inayofanya vilabu vingi vikubwa duniani kubadili muundo wa jezi kila msimu, ni kusaidia klabu iweze kufanya biashara ya mauzo ya jezi kwani mashabiki wengi wa soka barani Ulaya huwa wanajivunia kuvaa na kumiliki jezi orijino ya klabu anayoipenda.

Shabiki wa klabu husika anaona fahari kuvaa jezi orijino na anajivunia pia, kuna vilabu ambavyo vimeshatangaza aina ya jezi watakazotumia msimu ujao ikiwemo Arsenal na sasa ni zamu ya Chelsea mtu wangu, nimekuwekea video ya jezi za Chelsea watakazotumia msimu ujao kwa mechi za  nyumbani.
Msanii Linah Sanga alimaarufu kama Ndege mnana amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye nje ya kazi yake ya sanaa ni msusi mzuri............... by j.twice

wa nywele na alikuwa akifanya kazi hiyo toka akiwa shuleni na anaipenda hivyo anadai mpaka sasa bado anaipenda na anazidi kujifunza mambo mbali mbali yanayohusu urembo na ususi sababu ni kitu anachokipenda.
Linah alisema kuwa kipindi alipokuwa shule alikuwa maarufu sana kwa ususi kwa kuwasuka watu nywele ingawa alikuwa analipwa ujira mdogo wa shilingi mia tano lakini alikuwa anapenda kile alichokuwa akikifanya na alikuwa anafurahi kuona anawasuka wanafurahi kusukwa vizuri na yeye.
Unajua mimi napenda sana ususi toka nikiwa shule nilikuwa nawasuka wenzangu ingawa walikuwa wakinilipa pesa ndogo Shilingi mia tano lakini nilikuwa napenda kuwasuka na walikuwa wanapendeza hivyo hali hiyo iliendelea hata nilipokuwa nyumbani kuna watu nilikuwa nawasuka hivyo kusuka ni kipaji changu nje ya muziki nao fanya sasa, najitahidi sana niweze kuwa na Salaoon yangu.
"Unajua mimi jina langu kwa sasa ni kubwa na thamani yake pia hivyo siwezi kusema nifungue tu kiji-Saloon bali napaswa kufungua Saloon kubwa yenye sifa la jina langu, kiasi kwamba hata mtu akiangalia na kuaambiwa hii Saloon ya Linah aweze kukubali na kuona yes nimefanya jambo, ndiyo maana nasema inabidi nijipange kwanza ili niweze kufanya hilo.
Linah anakiri wazi kuwa ususi ni kipaji chake lakini anasema kutokana na kuwa busy na masuala ya muziki kipaji chake hicho cha ususi kimekaa pembeni japo anaamini kuwa anaweza kukiendeleza na kufanya mwenyewe hiyo kazi na kwenda sawa na mabadiliko ya mitindo ya nywele yaliyopo kwa sasa
" Ingawa kwa sasa kuna style nyingi za ususi hivyo naamini hazinitoi jasho inabidi kujifunza tu na kufanya sana mazoezi ila ninaweza kujifunza na kuvijua vitu vingine vingi zaidi vinavyohusiana na ususi na mambo ya urembo kama nitajifunza na kujiongeza " Aliongeza Linah Sanga
Nyumba ya nyota wa muziki Chris Brown kutoka Marekani imevamiwa na kupekuliwa na watu watatu waliofunika nyuso zao ambao walimfungia shangazi lake ndani chumba chake kulingana na maafisa wa polisi.
Nyota huyo wa muziki wa R&B hakuwepo nyumbani kwake wakati wa wizi huo ambao ulifanyika alfajiri siku ya jumatano.
Maafisa wanasema kuwa washukiwa ambao walikuwa na bunduki waliondoka katika jumba hilo la Tarzana na fedha za kiasi kisichojulikana pamoja na vitu kadhaa vya kibinafsi.
Brown au wawakilishi wake bado hawajatoa tamko lolote kuhusu tukio hilo.

Chris Brown na Rihanna kabla ya wawili hao kukosana
Kulingana na ripoti,nyota huyo alikuwa ameenda kujivinjari katika kilabu moja wakati wa kisa hicho
Hii ni mara ya pili ya nyumba ya msanii huyo ambaye alikuwa mpenziwe nyota wa muziki wa Pop Rihanna kuvamiwa katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni.
Mnamo mwezi Mei,aliwasili nyumbani na kumpata mwanamke mmoja aliyedaiwa kuvunja na kuingia kupika vyakula kadhaa na kuandika ukutani kwamba anampenda msanii huyo.by j.twice

Wednesday, July 15, 2015

BADNEWS KWA WASHIKA MITUTU WA LONDON!!!!! By j.twice
Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez atakosa mwanzo wa msimu baada ya kuisaidia Chile kunyakua ubingwa wa Copa America. Sanchez, 26, alipachika mabao 25 msimu uliopita na kuisaidia Arsenal kumaliza katika nafasi ya tatu.
Wenger amesema: "Alexis atarejea Agosti 3. Aghalabu huchukua wiki tatu kuwa tayari kwa mchezo. Bila Alexis tutakuwa pungufu kidogo. Bila shaka atakosa mchezo wa kwanza."
Hii inamaanisha Sanchez atakosa mechi ya Ngao ya Hisani dhidi ya Chelsea Agosti 2 na pengine mechi ya kwanza ya Arsenal ya Ligi Kuu dhidi ya West Ham wiki inayofuata.


Tuesday, July 14, 2015

Alex Ferguson amewashangaa Juventus kwa kufanya maamuzi haya… By J.twice

Kocha wa zamani wa klabu ya Manchester United ya Uingereza Sir Alex Ferguson ameshangazwa na uamuzi wa klabu ya Juventus ya Italia kusuasua kufanya maamuzi ya kumuuza kiungo wake Paul Pogba katika klabu ya Fc Barcelona ya Hispania.

Ferguson anaamini ingekuwa busara zaidi kama klabu ya Juventus ingemuuza kiungo huyo katika klabu ya Fc Barcelona ambao wameonyesha dhamira ya dhati ya kumuhitaji nyota huyo raia wa kifaransa.



Watendaji wa Fc Barcelona na watendaji wa Juventus walikutana wiki  iliyopita na kukubali kutoa kiasi cha zaidi ya poundi million 50 kama ada ya uhamisho wa Pogba,kitu ambacho Ferguson anaamini walifanya makosa kukataa ofa hiyo.

 Alitamani Facebook ya bure..kilichomkuta ni stori nyingine!! By J.twice


Mitandao wa kijamii imeendelea kupata mashabiki wengi duniani na imesaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha mawasiliano baina ya watumiaji wake.

Pamoja na faida tuna zozipata kupitia mitadano kuna wale wengine ambao wamejikuta ikiwadhuru wakiwemo wale ambao hutamani kupata selfie za peke yao ambao wengine imewapelekea kupoteza maisha.

Kuna hii imetokea Romania, ambapo binti wa miaka 14 amepoteza maisha baada ya kukaa juani kwa muda mrefu wakati akitumia mtandao wa Facebook.

Andreea Patuleanu alipoteza maisha baada ya kupata ugonjwa wa kiaharusi uliosababisha apoteze maisha baada ya kukaa juani muda mrefu  ili aweze kupata mtandao wa facebook bure.

Polisi wa Romania walisema binti huyo alitumia muda mwingi kukaa juani kabla ya kupoteza maisha ikiwa ni baada ya kushindwa kumudu gharama za kujiunga na mtandao huo kwa kulipia.
 50 Cent kafikishwa Mahakamani na anadaiwa faini, ni kweli amefilisika?? By j.twice

Kumekuwa na stori nyingi kuhusiana na rapper 50 Cent kutoka Marekani, moja kubwa kuhusu yeye ilikuwa ni stori inayohusiana na yeye kuvijisha video ya ngono ya mwanadada Lastonia Leviston ili kumuaibisha mshindani wake kwenye muziki, Rick Ross.

Kesi ikaenda Mahakamani na hukumu inaonesha 50 Cent anatakiwa alipe faini ya dola Mil.5 sawa na Billioni 10 za Kitanzania kwa mwanadada huyo.



Headlines za 50 Cent leo ziko tofauti, Mwanasheria wa rapper huyo ametangaza kwamba jamaa kafilisika, Mahakamani zimepelekwa document zinazoonesha kuwa 50 Cent ana madeni yasiyopungua dola Mil.50 sawa na Bil.100 za Kitanzania.



Sheria inatoa nafasi kwa mtu kupeleka Mahakamani documents na vielelezo vingine vinavyompa nafasi kujilinda na kuokoa baadhi ya biashara zake wakiwa wanakabiliana na madeni makubwa.

Msemaji wa mwanasheria wa 50 Cent, Travis Carter amesema msanii huyo amelazimika kufanya hivyo kuweka mambo yake ya kiuchumi sawa lakini hii haimanishi rapper huyo hana uwezo wa kusimamia biashara ama pesa zake.



Kwenye Interview moja 50 Cent alisema: “Kufanya hivi kunanilinda mimi na maslahi yangu ya biashara nyingi ninazojihusisha nazo, ni kawaida kwa wafanyabiashara kufanya hivi ni sawa na kulinda mifuko yangu. Uwezo ninao sema narekebisha tu vitu fulani kwa faida yangu na wadeni wangu”>>> 50 Cent.



Travis Carter alisema: “Maslahi yake ya kibiashara yataendelea kama kawaida na ataendelea kujihusisha na biashara zake nyingine na kuendelea kufanya kazi kama entertainer”.



Kwa sasa rapper 50 Cent anaishi Connecticut Estate kwenye nyumba aliyoinunua kutoka kwa bondia wa zamani, Mike Tyson mwaka 2003.
 Iyanya kwenye headlines tena, karudi na hii video mpya: “Applaudise!” By j.twice


Msanii maarufu kutoka Nigeria Iyanya anaziandika headlines za leo kwenye kurasa za burudani. Baada ya kudondosha video ya Nakupenda alioshirikiana na Bongo Superstaa Diamond Platnumz leo hii amerudi na kichupa kipya.



Wimbo unaitwa  Applaudise na hapa nimekusogezea video yake. Bonyeza play kuitazama
 Lil Wayne karushiwa chupa na Birdman night club akashtukia.. tukio lilirekodiwa kwenye hii video. By j.twice
Kwa muda mrefu sasa hivi kumekuwepo na beef kati ya rapper Lil Wayne na Birdman wa Cash money na hii ni baada ya Wayne kujitoa Cash Money kwa kutoridhishwa na ishu kadhaa ikiwemo kutosikilizwa anachotaka hasa kwenye ishu ya album yake kucheleweshwa kutoka.



Picha za tukio lenyewe, Lil Wayne akishangaa kurushiwa chupa alafu kwenye hii ya kulia ndio birdman anaonekana na timu yake.

Baada ya kujitoa Cash Money, Wayne ameendelea na show zake kama kawaida ambapo weekend iliyopita alikuwepo Miami Marekani kwenye club moja ya usiku ambapo kumbe na ‘mbaya wake’ Birdman nae alikuwepo tena akimtazama Lil Wayne kwa chini wakati akiperform.

Inadaiwa Birdman alirusha kwa Lil Wayne chupa ya kinywaji alichokua anakunywa na kusababisha show kusimama kwa sekunde chache huku watu wakijiuliza chupa imetoka wapi lakini badae ndio ikaja kujulikana kwamba Birdman ndio aliirushA chupa hiyoo

Monday, July 13, 2015

Cheki halo kichupa kipya cha digna kutoka JJ band wakishirikiana vizuri na maromboso kutoka kundi la ya moto band kwa mkubwa was wanae unann   cha kusemaa juu ya kichupa hiki 

Sunday, July 12, 2015

Kwa aliye zaliwa siku ya Leo ni kwamba kuwa amezaliwa siku moja na Bonge moja la presenter Dada mkubwa shadee ee tokea kituo chako bora cha matangazooo clouds FM and clouds TV .watazamaji wa clouds TV watakuwa wanamjua sawasawaa huyooo hapooo nimekusogezea
Nimekusogezea hapa remix ya Wizkid ft drake

Saturday, July 11, 2015

Breaking News: Bastian Schwesteiger athibitishwa kwenda Man United – awek rekodi hii By j.twice
Klabu ya Manchester United imekubaliana kimsingi na mabingwa wa Bayern Munich juu ya usajili wa kiungo wa timu ya taifa ya Ujerumani Bastian Schweinsteiger.

  Bastian, mwenye umri wa miaka 30, aliomba mwenyewe klabu ya Bayern Munich kutompa mkataba mpya na angependa kwenda sehemu nyingine.

Mkurugenzi mkuu wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge ameongea na waandishi wa habari muda mfupi uliopita na kusema: “Marafiki zangu wa pale Manchester United tumekuwa na mawasiliano kwa muda kidogo. Tumefikia makubaliano juu ya uhamisho wa Bastian.

Schweinsteiger ameshaichezea Bayern Munich mechi 536 tangu alipovaa jezi ya timu hiyo kwa mara ya kwanza mwaka 2002.

 
Inamaanika kwamba Bastian amevutiwa kujiunga na Manchester United kutokana na kuwa na mahusiano mazuri na kocha Louis van Gaal ambaye alimfundisha soka wakati alipokuwa kocha wa Bayern Munich.

Ada ya uhamisho iliyolipwa kumsajili Schwesteiger inaaminika kuwa karibia kiasi cha £8m na mshahara wake utakuwa kiasi cha £7m kwa mwaka.

AYOTV AyoTV: Lulu amejibu kwanini aliifuta account yake ya Instagram? ni noma je? By Millard Ayo and j.twice
Mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ alikua na time ya kukaa mbele ya camera ya AyoTV na kuzungumzia ishu kadhaa ikiwemo movie yake mpya inayokuja lakini pia aliulizwa swali la kwanini aliifuta page yake ya Instagram ambayo ilikua ina followers zaidi ya laki tatu.
Manchester yapata sahihi ya mchezaji wa Torino ya Italy Matteo darmian na hapa nimekusogezea uwone ufundi wake je anafaa kuchezea united

Wednesday, July 8, 2015

’.. Video mpya kutoka kwa Bracket Feat. Tecno By J.twice


Kundi la Bracket kutoka Nigeria waliachia ngoma ya ‘Alive’ Feat. Diamond Platnumz & Tiwa Savage.. ni hit ambayo ilishika sana kwenye TV na radio kubwa Afrika.

Jamaa wamerudi tena mtu wangu, wameachia video yao mpya inayoitwa ‘Panya’ alieshirikishwa hapo anaitwa Tecno.

Bracket Feat. Tecno– ‘Panya’ yenyewe ndio hii hapa sasa.





Monday, July 6, 2015


 Drogba awataja mabeki hawa kuwa ndio waliomsumbua zaidi dimbani By j.twice
Gwiji wa zamani wa soka la kimataifa wa Ivory Coast na klabu ya Chelsea Didier Drogba, ni mmoja wa washambuliaji bora zaidi waliowahi kutamba katika barani Afrika, Asia na Ulaya.

Drogba ambaye alitangaza kustaafu kuichezea Ivory Coast mwaka jana, pamoja kufahamika kuwa mwiba mkali kwa mabeki wa timu pinzani wakati akiwa kwenye ubora wake, Drogba pia nae alikuwa na mabeki ambao walikuwa ni visiki zaidi kila alipokuwa anakutana nao.

  Didier Drogba amemtaja nahodha wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Spain – Carles Puyol, Rio Ferdinand, na Nemanja Vidic kuwa ndio mabeki visiki zaidi aliowahi kukutana nao.

Akizungumza katika mahojiano yake na Rio Ferdinand, Didier Drogba alisema:.
  “Siku zote nimekuwa nikisema wewe Rio na Vidic ni walinzi ambao nilikuwa napata sana taabu timu zetu zinapokutana. Nilipokuwa nikifunga dhidi ya Manchester United nilikuwa nafurahia sana kwa sababu si mara nyingi nilikuwa nikipata nafasi ya kufunga dhidi yao.

“Hivyo, nyie wawili na Carles Puyol ndio mabeki ambao mlinisumbua sana – Carles alikuwa mzuri sana uwanjani na hata nje.”
Pombe imeandikwa kabisa #RestInPeace na jeneza pembeni.. wako wanaoitumia kabisa !! By j.twice


Kenya imetajwa kwenye Top Ten ya nchi Tajiri Afrika 2015, hiyo ni good news.. Zimebaki wiki kama tatu hivi ili tushuhudie Rais wa Marekani, Barrack Obama anatembelea nchi hiyo, hiyo ni good news.. lakini ziko story upande wa pili wa shilingi pia.

Kama wewe ni mtazamaji wa Taarifa za Habari kwenye TV za Kenya itakuwa umeshuhudia pia majanga ya pombe za kienyeji, wapo wanaofariki, wengine wanajikuta hali mbaya mpaka wanalazwa Hospitali, lakini bado kuna wengine wanaendelea kutumia vilevile!!


Huyu ni mmoja ya watu waliozidiwa na kujikuta hawana hata nguvu ya kuinuka kutembea.

Moja ya vitu vilivyonishtua ni hii kukutana na chupa ya Pombe ambayo wanasema hata haijasajiliwa na inauzwa kama kawaida. jina lake je? >> Inaitwa ‘Rest in Peace Premium Vodka‘ na kuna picha ya Jeneza kabisa kwa chini yake.
 Swali likamchefua Christiano Ronaldo, kawaacha waandishi wa habari kwenye mataa..(Video) By j.twice
Mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo ametoa kali  baada ya kuondoka katikati ya kipindi cha runinga wakati akihojiwa na Televisheni ya Sports News.

Kitendo cha mchezaji huyo kuondoka kulisababishwa na kuulizwa swali kuhusu mchezaji mwenzake beki Sergio Ramos. kama ataendelea kubaki Real Madrid au kujinga na Manchester United swali lililoonekana kumkera.



Ronaldo alijibu hajui lolote lakini gafla alitoa headphones shingoni na kumshukuru mtangazaji kisha kuondoka zake kabla kipindi hakijamalizika.
Meek Mill na Future washirikiana kukuletea video hii mpya: Jump Out The Face. By j.twice


Baada ya kutumbwiza kwenye tuzo za BET Awards mwaka huu na kudondosha album yake mpya ya Dreams Worth Than Money, Meek Mill ameanza wiki hii na video mpya ya wimbo wake Jump tOut The Face aliomshirikisha msanii mwengine wa Hip Hop Future.

Meek Mill anategemea kuungana na girlfriend wake Nicki Minaj kwenye tour yake ya PinkPrint Tour itakayo anza rasmi jijini Dallas tarehe 17 mwezi huu.

Nimekusogezea video hiyo hapa  mtu wangu bonyeza Play kuitazama.

Sunday, July 5, 2015

Nimekusogezea wimbo mpya wa Kendrick Lamar: Alright. (Video) By  J.twice


Kendrick Lamar ni msanii wa HipHop ambaye anatamba na album yake mpya iitwayo Pimp A Butterfly, album ambayo inafanya vizuri Marekani. Kendrick ameona asikae kimya sana, ameamua atusogezee video mpya ya wimbo unaopatikana katika album hiyo.







Rais Kikwete kuhusu Wanasiasa wanaomwaga fedha! By j.twice
Rais JK.

Yafuatayo ni maneno kwenye mistari tofauti iliyoandikwa na Rais Jakaya Kikwete ikiwa ni miezi mitatu tu imebaki Tanzania kuingia kwenye uchaguzi mkuu wa Rais na Wabunge.

Hii ni tweet ya kwanza aliandika July 4 2015 >>> ‘Utaratibu bora wa kuchagua kiongozi wa nchi si wa kuanza kujadili majina, bali wa kuanza kujadili changamoto na vipaumbele vya Taifa kwanza‘

Tweet alizoandika July 5 2015 >>> ‘Tusiwasikilize wanasiasa wanaowagawa Watanzania na kutumia fedha kutafuta madaraka. Mchezo wao ni mauti yetu. Wakatalieni kwa macho makavu, Tusiruhusu wanasiasa kutumia dini ambazo ni mhimili muhimu wa amani yetu. Ukiwepo mfarakano wa kidini hakuna mtu wala eneo litakalonusurika’

Mstari mwingine ameandika >>> ‘Tukiamua kwa utashi wetu kuzipoteza tunu za amani na upendo, katu hatuwezi kusema ni mapenzi ya Mungu bali itakuwa ni makosa yetu wenyewe, kiongozi wa dini anapaswa kukumbusha wajibu wa: kujiandikisha, kupiga kura na kuchagua kiongozi bora; si kuwaambia waumini wamchague fulani‘

AYOTV Video ikionyesha walichokifanya Abdu Kiba na Ruby nyuma ya Camera! By Millard Ayo and j.twice team Millard ayo

Ni dakika chache ambazo zinakutangulizia kuona kitachofata kwenye video mpya ya Abdu Kiba ft. Ruby (Ayaya) ambayo ni single mpya kwenye radio kwa wiki kadhaa sasa hivi.

Location ya hii video ni White Sand Dar es salaam Tanzania.
Everybody On The Floor (Audio) By j.twice

Msanii maarufu kutoka kwenye lebo ya G-Unit The Game leo ameachia single yake mpya iitwayo Everybody On The Floor, ndani msanii kutoka Atlanta Migos amesikika. Kama bado  hajapata nafasi ya kuisikiliza ngoma hiyo

 Uamuzi mgumu wa uongozi wa Shirikisho la soka Nigeria kwa kocha wa timu ya Taifa… By J.twice



Shirikisho la soka Nigeria NFF baada ya kupitiwa taarifa za Kamati ya Nidhamu, Ufundi na Maendeleo. limefikia uamuzi wa kumtimua kazi kocha mkuu wa timu ya Taifa ‘Super Eagles’, Steven Keshi kuendelea kuifundisha timu hiyo.

Makamu wa kwanza wa Rais wa NFF, Seyi Akinwunmi amewahakikishia Wanigeria kwamba uamuzi huo haujachukuliwa kwa kukurupuka, bali umezingatia maslahi ya soka ya Nigeria.

Keshi, ambaye ni Nahodha wa zamani Super Eagles amekuwa kocha wa timu ya taifa kwa vipindi vitatu tofauti kati ya mwaka 2011 na 2015, na mafanikio yake makubwa yakiwa ni kuwapa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2013 Afrika Kusini na kufika Raundi ya Pili katika Kombe la Dunia mwaka jana Brazil.

Kocha huyo amefukuzwai ikiwa ni miezi miwili kabla ya Nigeria kusafiri kuja Tanzania kumenyana na Taifa Stars katika mchezo wa kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika yatakayofanyika mwaka 2017.

Saturday, July 4, 2015

 Jamaa kalikimbia begi lake ndani ya basi, hiki ndio ambacho Askari wamekuta ndani !! (Picha & by j.twice

Mara nyingi tunasikia stori kuhusu watu kukamatwa na dawa za kulevya kwenye viwanja vya ndege, wapo wanaotoka TZ kwenda nje na wapo wanaokamatwa wanaziingiza pia kutoka nje ya nchi.. nina hii stori kutoka ITV kuhusu mtu kukutwa na bangi ndani ya basi.



Basi la Maning’inice lilitoka Mtwara kwenda Dar, njiani kulikuwa na Checkpoint ya Polisi ambapo jamaa aliyebeba bangi kwenye begi aliomba akajisaidie, Polisi walipoingia kwenye gari kukagua wakakutana na begi hilo lililojaa bangi na jamaa mwenye nalo alikuwa ameshakimbia tayari.



“Kuna mtu mmoja aliteremka akasema ana mkojo.. Askari akauliza nani mwenye hili begi yule jamaa akaanza kukimbia vichakani. Askari wakakimbizana nae maporini, akatokomea“– amesimulia dereva wa basi hilo, Hashim Mohamed.
 Breaking News: Baada ya kuondoka Man Utd, Falcao arudi tena kucheza EPL By j.twice
Miezi takribani miwili baada ya klabu ya Manchester United kuamua kutoendelea kupokea huduma za Radamel Falcao kwa kutompa mkataba wa kudumu, mchezaji huyo wa Colombia amepata timu mpya ndani ya ligi kuu ya Uingereza.
Falcao ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Colombia, anatarajia kujiunga na Chelsea kutokea Monaco kwa mkataba wa mwaka mmoja wa mkopo.

Mchezaji huyo msimu uliopita alisajiliwa na Manchester United kwa mkopo wa mwaka mmoja na endapo angewaridhisha benchi la ufundi la klabu hiyo kwa kiwango kizuri basi angesajiliwa kwa mkataba wa kudumu, hata hivyo hakufanikiwa kumshawishi Louis Van Gaal kumpa mkataba huo.

  Sasa anajiunga na Jose Mourinho, kocha ambaye amekuwa hafichi mapenzi yake mbele ya mchezaji huyo ambaye alijaribu kumsajili kwa muda mrefu bila mafanikio.
Eminem amerudi na ngoma mpya Kings Never Die, pembeni Gwen Stefani.(Audio) By j.twice




Msanii wa Hip Hop Marekani Eminem alikuwa kimya kwa muda lakini sasa amerudi tena kuziandika headlines zake kwenye ubao wa burudani. Eminem ameachia ngoma mpya wiki hii, ndani kamshirikisha msanii mwengine maarufu wa muziki wa Pop RnB Gwen Stefani.

Wimbo unaitwa Kings Never Die, na unaweza kuisikiliza hapa






 Wabunge wengine 35 nao wamepigwa stop kuingia Bungeni kwa siku tano
By .j.twicee

Kumekuwa na story nyingi tofauti toka ndani ya Kikao cha Bunge Dodoma, kwa muda wa siku tatu mfululizo zimetokea vurugu, Kikao kikaahirishwa kwa siku mbili mfululizo.

Alhamisi July 02 2015 Mbunge John Mnyika aliomba mwongozo kuomba Bunge lisiendelee kwa vile ishu ya kujadili Miswada mitatu kwa siku moja ilikuwa inakiuka Kanuni za Bunge, ukatokea mvutano na baadae Spika AnneMakinda akaahirisha Bunge.


Spika wa Bunge, Anne Makinda.

Ijumaa July 03 2015 hali ikawa hivyohivyo tena, wakati Waziri George Simbachawene anasoma Muswada, ikatokea mvutano mwingine, zikaanzishwa kelele Bunge likaahirisha tena.. Kikao cha Jioni Spika Anne Makinda akarudi na list ya majina ya Wabunge ambao wamesimamishwa Bungeni kutokana na maamuzi ya Kamati ya Maadili ya Bunge.



Leo July 04 2015 Kikao kimeanza tena saa tatu asubuhi, Mbunge Ezekiel Wenje akaomba Spika atoe ufafanuzi wa kwanini Mbunge Silinde hayuko kwenye list ya waliotajwa kusimamishwa lakini Askari wa Bunge wamemzuia asiingie kwenye Kikao?

Majibu ya Spika hayakuwaridhisha baadhi ya Wabunge, zikaanza tena kelele… Spika akataja list ya Wabunge wengine ambao wanasimamishwa kuhudhuria Vikao vya Bunge kwa siku tano kila mmoja.

List ya Wabunge wote iko hapa.

Ezekiel Wenje

Mussa Kombo

Masoud Abdallah Salim

Rebecca Ngodo

Sabrina Sungura

Khatib Said Haji

Dr. Anthony Mbassa

Maulidah Anna Valerian Komu

Kulikoyela Kahigi

Cecilia Pareso

Joyce Mukya

Mariam Msabaha

Grace Kiwelu

Israel Natse

 Mustapha Akonaay

Konchesta Rwamlaza

Suleiman Bungura

Rashid Ali Abdallah

Ali Hamad

Riziki Juma

Rukia Kassim Ahmed

Azza Hamad

Khatibu Said Haji

Kombo Khamis Kombo

Ali Khamis Seif

Haroub Mohammed Shamisi

Kuruthum Jumanne

Mchuchuli

Amina Mwidau

Mkiwa Kimwanga

Salum Baruhani

Marry Stellah Malaki

Rashid Ally Omary

Mwanamrisho Abama

Lucy Owenya

Thursday, July 2, 2015

oi Hiyo ni interview ya august alsina kuhusu albam yake ni shidaaa
Gari laingia katika paa ya nyumba south afrika by j.twice



Mapema jana gari liligonga na kuingia ndani ya nyumba moja nchini Afrika Kusini kupitia paa la nyumba hiyo kulingana na huduma ya dharura ya ER24 nchini humo.


Dereva wa gari hilo amesema kuwa alipokuwa akiliendesha gari hilo alikutana na tuta moja barabarani lililosababisha gari hilo kuruka na kuanguka katika paa la nyumba hiyo.


Bado haijulikani ni vipi tuta hilo lilisababisha ajali hiyo.
Hakuna mtu aliyejeruhiwa na dereva wa gari hilo hakupata jeraha lolote.