By .j.twice
Louis van Gaal amekiri Javier Hernandez 'Chicharito' atapata nafasi nyingine ya kupigania nafasi yake kwenye Kikosi cha Manchester United akiungana na Timu hiyo hapo Julai 25 huko Ziarani Marekani.
Chicharito, ambae aliifungia Man United Bao 59 katika Mechi154, alipelekwa kwa Mkopo huko Real Madrid Msimu uliopita baada Van Gaal kuamua atakuwa nyuma ya Wayne Rooney, Robin van Persie na Radamel Falcao katika kupewa namba.
Lakini, baada ya Man United kuifunga Club America 1-0 mapema Leo, Van Gaal aliulizwa hatima ya Chicharito na kueleza: "Chicharito anakuja Julai 25. Ana nafasi ya kudhihirisha uwezo wake hasa baada ya Falcao na Van Persie kuondoka, hivyo nafasi yake kubwa."

No comments:
Post a Comment