Tuesday, July 14, 2015

Alex Ferguson amewashangaa Juventus kwa kufanya maamuzi haya… By J.twice

Kocha wa zamani wa klabu ya Manchester United ya Uingereza Sir Alex Ferguson ameshangazwa na uamuzi wa klabu ya Juventus ya Italia kusuasua kufanya maamuzi ya kumuuza kiungo wake Paul Pogba katika klabu ya Fc Barcelona ya Hispania.

Ferguson anaamini ingekuwa busara zaidi kama klabu ya Juventus ingemuuza kiungo huyo katika klabu ya Fc Barcelona ambao wameonyesha dhamira ya dhati ya kumuhitaji nyota huyo raia wa kifaransa.



Watendaji wa Fc Barcelona na watendaji wa Juventus walikutana wiki  iliyopita na kukubali kutoa kiasi cha zaidi ya poundi million 50 kama ada ya uhamisho wa Pogba,kitu ambacho Ferguson anaamini walifanya makosa kukataa ofa hiyo.

No comments:

Post a Comment