Tukiwa tunasubiri kuanza kwa Ligi Kuu Uingereza msimu ujao vilabu kadhaa vimekuwa vikitangaza jezi za mechi za nyumbani na ugenini… Mara nyingi jezi zao huwa hazibadiliki rangi kinachobadilika ni muundo tu wa jezi na wakati mwingine nembo ya mdhamini kutegemeana na Mkataba ambao Klabu wanao.
Sababu mojwapo inayofanya vilabu vingi vikubwa duniani kubadili muundo wa jezi kila msimu, ni kusaidia klabu iweze kufanya biashara ya mauzo ya jezi kwani mashabiki wengi wa soka barani Ulaya huwa wanajivunia kuvaa na kumiliki jezi orijino ya klabu anayoipenda.

No comments:
Post a Comment