Mchezaji aliyetokea ligi daraja la kwanza na kufanya Yanga iwaite Waandishi wa habari By j.twice
Baada ya Uongozi wa Klabu ya Kimondo inayoshiriki ligi daraja la kwanza kudai mshambuliaji GEOFREY MWASHIUYA ni mali yao, Yanga imemtambulisha rasmi mshambuliaji huyo baada ya kukamilisha usajili wake.
Kimondo kupitia kwa Mkurugenzi ERICK AMBAKISYE wameshangazwa na hatua ya Yanga kumtumia mshambuliaji huyo kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Sports Club Villa ya Uganda Jumamosi iliyopita wakidai kuwa bado ni mchezaji wao.
Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Yanga JERRY MURO anasema MWASHIUYA ni mchezaji wao halali kwa sababu wamemsajili kwa kufuata taratibu zote.
Jerry Muro amesema ‘Geofrey amejitokeza hadharani amecheza mpira watu wakaanza kushtuka baada ya kuona dhababu imeanza kung’ara mimi nikashangaa, alikua anakaa hapa akaenda kuishi Tabata….. tumekaa nae muda huo wote, watu walikua wapi wasiseme ni mchezaji wao?’
‘Niwataarifu kanuni sheria na taratibu, mchezaji anapochezea ligi daraja la kwanza mchezaji mkataba wake unakwisha pale ligi inapokwisha, hata kama angekua na mkataba wale wa kule daraja la kwanza hawana mikataba ya miaka mitano au mitatu‘ – Jerry Muro
‘Tumekwenda TFF na kuuliza… hana mkataba na Kimondo, zile wanazosema ni fomu ambazo mchezaji anajaza ili acheze ligi daraja la kwanza apate kitambulisho kama zilivyo taratibu nyingine‘ – Jerry Muro
Tuesday, June 30, 2015
Mwimbaji wa longtime kwenye muziki wa dance Tanzania Banza Stone alikutana na Waandishi wa habari wachache kwa ajili ya kukanusha taarifa za kuzushiwa kifo, maisha yake kwa sasa na kilichokua kinamsumbua kiafya.
Maneno ya utani ya Rais Mugabe kwa Obama baada ya kuruhusu ndoa ya jinsia moja… By J.twice
Ndani ya wiki moja baada ya Serikali ya Marekani kupitisha Sheria ya kuruhusu Ndoa za jinsia moja kwa raia wake kumekuwepo na maoni mbalimbali kutoka kwa watu kuhusiana na maamuzi hayo.
Mmoja wa watu walioguswa na maamuzi hayo ni Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe ambaye ameeleza hisia zake baada ya maamuzi hayo kupitishwa.
Rais wa Marekani Barack Obama
Katika mahojiano na radio ya Taifa ya Zimbwabwe, Mugabe alisema hawezi kupingana na maamuzi ya nchi hiyo kwani ni sheria ambayo imepitishwa na Serikali na kama ni hivyo ataamua kufunga safari kwenda mpaka Washington kuomba kufunga ndoa na Rais Barack Obama.
Ameongeza kuwa, Serikali ya Marekani imekuwa ikiongozwa na wajinga ambao ni wafuasi wa shetani wanaoitukana taifa la Marekani akisisitiza Marekani imechafuka na wanaiendesha nchi kwa dhana zao binafsi ambazo ni potofu.

Yanga wamesajili hawa wawili leo, mmoja toka Ghana na mwingine toka Zimbabwe… (Pichaz) By j.twice
story za Ligi Kuu Tanzania Bara imeanza mdogomdogo mtu wangu, tunasubiri August 2015 ili tuzione Timu zote kali zikitoana jasho kwenye viwanja tofauti vya Soka TZ.
Magazeti ya Michezo TZ yana story nyingi, zipo Timu zilizoleta makocha wapya kwa ajili ya kujiandaa na ligi hiyo, wapo waliosajili wachezaji pia.. nimepita kwenye ukurasa wa Yanga na kukutana na story kwamba nao wameongeza vifaa vyao viwili, mmoja wao anatoka Zimbabwe na mwingine anatoka Ghana.majina ya wachezaji hao ni donald ngoma toka Zimbabwe na joseph zuttah alimaarufu kama tetteh tokea gnana

Baada ya Madrid kuikataa Ofa ya Man Utd, Ramos amefanya uamuzi huu By j.twice
Wiki moja baada ya ofa ya kwanza ya Manchester United kumsajili Sergio Ramos kukataliwa na Real Madrid, hatimaye mchezaji huyo ambaye yupo mapumzikoni ametoa kauli yake.
United walituma ofa ya kwanza ya paundi milioni 28.3 kwa Madrid ili kupata saini ya beki huyo wa kimataifa wa Spain, lakini Madrid waliikataa ofa hiyo.
Hata hivyo baada ya Ramos kugundua Madrid wameikataa ofa hiyo, alichukua uamuzi wa kuwaweka wazi viongozi wa Madrid kupitia wakala wake kwamba anataka kuondoka na kujiunga na United na kuiomba Madrid ikubaliane bei na Manchester United.
Uamuzi huo wa Ramos umeishtua Madrid, ambao walitegemea wangefanya makubaliano ya mkataba mpya na beki huyo.
Madrid wanategemewa kujaribu kumtuliza Ramos na mkataba mnono mpya lakini kaka na meneja wa mchezaji huyo, Rene Ramos ameshaifahamisha Madrid lengo la mteja wake kutaka kuanza maisha mpya sehemu nyingine.
Rene ameripotiwa kusema kwamba Ramos anataka kuhamia Old Trafford wakati huu wa dirisha la usajili na klabu pekee ambayo anataka Madrid ifanye nayo makubaliano ni United.

Hizi ndio sababu za Facebook kuamua kufungua office zao South Africa.. by j.twice
Nimeipata hii takwimu ambayo sikuwa nafahamu, kumbe Facebook ina watumiaji Milioni 120 wa Mtandao huo ndani ya Africa pekeyake !!
Story nyingine kuhusu Facebook kwa sasa hivi ni ishu ya kusogeza Office zao mpaka ndani ya Jiji la Johannesburg Afrika Kusini na tayari hapo ndio yatakuwa Makao Makuu ya shughuli zao zote zinazohusu Facebook Afrika, Nunu Ntshingila ndio Boss ambaye kachukua ajira kusimamia Kampuni hiyo
Mark Zuckerberg, Boss wa Facebook
Kingine ni kwamba jamaa wameamua kuisogeza Facebook ndani ya Afrika kama njia ya kusogea karibu ya wateja wao wengi ambao ni Wafanyabiashara wanaotumia Mtandao huo katika kutangaza biashara zao.
Facebook iliangalia siku nyingi sana jinsi ya kuingia kwenye soko la Afrika, waliwahi kurahisisha huduma kwa watumiaji wa mtandao huo kwa kuweka App maalum ambayo mtumiaji hakatwi pesa wala hatumii data kwenye kuchat, mpango wao mwingine ni kuhakikisha wanamfikia kila mtu hata ambae hana uwezo wa kumiliki simu yenye uwezo wa Internet.
Nunu Ntshingila, Boss wa Facebook Afrika.
Mpango walionao kwa sasa ni kuajiri wafanyakazi 25 ili ofisi ya Johannesburg ijitosheleze na kazi iendelee kama kawaida.

Juma Nature, mkongwe mwingine wa bongofleva mwenye tuzo ya kudumu ya heshima kwa ubunifu wa chorus ameshirikishwa kwenye single mpya na Riz Conc kupitia kwenye mikono ya producer Dupy ambaye amefanya kazi pia na watu kama Izzo B.
Monday, June 29, 2015
AJALI Picha 4 za ajali ya gari waliyoipata Nizar Khalfan na Shaban Kado By j.twice
Ajali imetokea Bahi Dodoma na kwenye gari miongoni mwa waliokuwemo ni pamoja na golikipa Shaban Kado na mchezaji Nizar Khalfan wa Mwadui FC na chanzo ni tairi la nyuma kuchomoka.
Kwenye interview Kado amesema hakuna yeyote aliyepoteza maisha isipokuwa majeraha waliyoyapata akiwemo Shaban Kado ambaye ameumia pia mkono wake wa kulia ambapo walikua watu wanne ndani ya gari.picha na Millard ayo

Tuzo za BET 2015 zimeshatolewa tayari, list yote ya washindi ninayo hapa! By j.twice
onJune 29, 2015 304SHARES COMMENTS
Tuzo za BET Awards 2015 zilichukua headlines kubwa siku ya jumapili tarehe 28 June 2015 Los Angeles Marekani ambapo mc alikua ni Anthony Anderson na Trace Ellis Rose.
Wakali wa muziki kama Chris Brown, Nicki Minaj, na Rihanna na wengine walimiliki stage kwa kuperform. Janet Jackson pamoja na Smokey Robinson walikua baadhi ya watu waliopewa tuzo za heshima mwaka huu na BET.
Hapa chini nimekusogezea orodha kamili ya wale wakali wote waliopokea tuzo ya BET Award mwaka huu wachache wakiwemo Beyonce akiongoza na tuzo 3, Nicki Minaj akiwa na 2, Kendrick Lamar, Big Sean, Chris Brown, John Legend wakiwa na tuzo moja kila mmoja na kwenye kile kipengele cha International Best Act: Africa Stonebwoy kutoka Ghana aibuka kidedea
Hii hapa ndio orodha kamili ya wasanii wote waliopokea tuzo za BET Award, karibu uitazame mtu wangu.
Best International Act UK:
FKA Twigs
Fuse ODG
Lethal Bizzle
Little Simz
Mnek
Stormzy- Winner
Best International Act Africa:
AKA
Stonebwoy- Winner
Sarkodie
Fally Ipupa
Sauti Sol
Wizkid
The Soil
Yemi Alade
Best Female R&B/Pop Artist:
BeyoncƩ- Winner
Janelle MonƔe
Jhene Aiko
Ciara
Rihanna
K. Michelle
Best Male R&B/Pop Artist:
Chris Brown- Winner
Trey Songz
The Weekend
August Alsina
Usher
John Legend
Best Group:
A$AP Mob
Migos
Rae Sremmurd- Winner
Rich Gang
Young Money
Jodeci
Best Collaboration:
Chris Brown Ft. Lil Wayne and Tyga – “Loyal”
Big Sean Ft. E-40 – “IDFWU”
August Alsina Ft. Nicki Minaj – “No Love”
Chris Brown Ft. Usher and Rick Ross – “New Flame”
Common and John Legend – “Glory”- Winner
Mark Ronson Ft. Bruno Mars – “Uptown Funk”
Best Male Hip-Hop Artist:
Kendrick Lamar- Winner
Common
Big Sean
Drake
J. Cole
Wale
Best Female Hip-Hop Artist:
Azealia Banks
Dej Loaf
Iggy Azalea
Tink
Nicki Minaj- Winner
Trina
Video of the Year:
Beyonce – “7/11”- Winner

Common and John Legend – “Glory”
Nicki Minaj – “Anaconda”
Video Director of the Year:
Benny Boom
Beyonce, Ed Burke and Todd Tourso – Winner
Chris Robinson
Fatima Robinson
Hype Williams
Best New Artist:
Bobby Shmurda
Dej Loaf
Fetty Wap
Rae Sremmurd
Sam Smith- Winner
Tinashe
Best Gospel Artist:
Michelle Williams
Erica Campbell
Deitrick Haddon
Fred Hammond
Mali Music
Lecrae- Winner
Best Actress:
Gabrielle Union
Kerry Washington
Taraji P. Henson- Winner
Tracee Ellis Ross
Viola Davis
Best Actor:
Anthony Anderson
Idris Elba
Jussie Smollet
Kevin Hart
Terrence Howard- Winner
Youngstars Award:
Jacob Latimore
Jaden Smith
Mo’ne Davis- Winner
Quvenzhane Wallis
Zendaya Coleman
Best Movie:
“Annie”
“Beyond the Lights”
“Selma” – Winner
“Think Like a Man Too”
“Top Five”
Sportswoman of the Year:
Brittney Griner
Candace Parker
Serena Williams- Winner
Skylar Diggins
Venus Williams
Sportsman of the Year:
Chris Paul
Floyd Mayweather Jr.
LeBron James
Marshawn Lynch
Stephen Curry- Winner
Viewer’s Choice Award:
The Weekend –“Earned It”
Kendrick Lamar – “I”
Dej Loaf – “Try Me”
Rae Sremmurd Ft. Nicki Minaj and Young Thug – “Throw Sum Mo”
Beyonce –“7/11”
Nicki Minaj Ft. Drake, Lil Wayne and Chris Brown – “Only” – Winner
Centric Award:
Avery Sunshine – “Call My Name”
Jazmine Sullivan Ft. Meek Mill – “Dumb”

Sam Smith Ft. Mary J. Blige –“Stay With Me”
The Weekend – “Earned It” -Winner.

Saturday, June 27, 2015
Steve Nyerere ametangaza rasmi anautaka Ubunge 2015, maneno yake ninayo hapa by j.twice
.
Aliyekuwa mwenyekiti wa Bongo Movie Unit, Steve Nyerere ameingia kwenye list ya wagombea ubunge mwaka 2015. Steve amesema ‘Kwanza ninataka kuwahakikishia watanzania sijakurupuka, nimekuwa mwanachama wa chama cha Mapinduzi umoja wa vijana almost miaka 25 na sasa hivi nina miaka 29 naelekea 30 lakini vilevile nimekuwa kamanda wa vijana miaka 10 tawi la bwani kinondoni, nimekuwa muhamasishaji wa chama cha mapinduzi kitaifa kwa muda wa miaka 10′
‘Sijakurupuka na wala sijatamkia sifa kwasababu labda nimeona mtu fulani amegombea, kinondoni kuna matatizo kadhaa nani anaweza kuyatetea hayo matatizo? nitakuwa mtetezi pamoja na matatizo ya wasanii wetu, kuhusu kazi zangu za filamu nitakuwa nafanya kama kawaida huku nikiwa natumikia kazi za Bungeni’
ATAACHA KUIGIZA?!
Amejibu >>> ‘Kazi yangu ya sanaa sitoweza kuiacha nadhani naweza kuwa ndio Mbunge wa kwanza yuko ndani ya Bunge na bado yuko kwenye sanaa anacheza filamu’
Peter na Paul Okoye kwa pamoja tunawajua kama P Square, ukubwa wa jina lao sio ndani ya Africa pekeyake… wana hits kibao ambazo zimewaweka kwenye ramaniya dunia pia.
Mafanikio yao yalianzia pale ambapo waliweka nguvu yao nyingi kwa kufanya muziki wakitumia lebo yao ya Square Records… December 2011 milango mingine mikubwa ikafunguka kwenye muziki wao, waliingia Mkataba kufanya kazi na lebo ya Akon Konvict Muzik.. kazi kama Beautiful Onyinye waliyomshirikisha Rick Ross na Chop My Money zilipenya sana nje ya Afrika, watu wakazidi kuwajua !!
Safari yao haikuwa rahisi, lakini unajua siri ya wao kuifungua milango yote ya mafanikio? Kuna kitu chochote wanachokihofia kwa sasa?
>>> “Siri ya mafanikio yetu ni kazi. Tunafanya sana kazi.. Juhudi zote tunazowekeza katika kazi yote ni hofu ya umaskini, tumeshaonja maisha ya umaskini mkubwa na tunaogopa sana umaskini, ndio maana utasikia tumewekeza hapa na kule yote ni kujikinga na umaskini.
Tumeshuhudia wasanii waliopata umaarufu na utajiri kabla yetu lakini leo hawana chochote cha kuonesha kwa juhudi zao, kitu hiki kinatuogopesha sana… Tuliwahi kuishi maisha ya kubanana baba, mama na watoto nane kwenye nyumba ya kupanga yenye vyumba viwili, chakula, ada, mavazi vilikuwa ni tatizo sana kwetu na kipindi hicho baba yetu alitusihi sana tuje kuwa viongozi wa maisha yetu wenyewe tusiopenda kufanya kazi chini ya mtu na ndio maana unawaona P Square wanafanya biashara zao wenyewe leo”.>>> Nukuu ya walichokisema P Square kwenye moja ya Interview.
Breaking News: Taarifa za magaidi Morogoro na picha za walivyokamatwa navyo. By j.twice
Kulikuwa na mfululizo wa uvamizi wa Vituo vya Polisi, watu wakapata hofu wengine walihusisha matukio hayo na ishu ya ugaidi baadae hali ikawa sawa.
Matukio hayajaisha, nimeipokea ripoti ya ITV kutoka Morogoro inayohusu watu watatu kufariki katika mapambano na Polisi, huku wawili kati yao wakihisiwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la Al Shabaab.
Breaking News nyingine kuhusu tukio hilihili iliyoripotiwa na Gazeti la Mwananchi inahusu watu sita kukamatwa na wengine 50 wanatafutwa, walikutwa wakiwa na sare za majeshi pamoja na silaha kama majambia kwenye msitu Mvomero.
Kwenye taarifa iliyofatia kutoka Mwananchi, imesema Mkulima Cassian Peter amefariki mchana wa June 27 2015 kwenye Hospitali ya Bwagala ambapo Polisi mmoja amelazwa na hii ni baada ya kujeruhiwa na hao watuhumiwa wa Ugaidi kabla hawajakamatwa.

Mzaliwa wa Tanzania Colonel Mustafa ni msanii wa siku nyingi kwenye muziki Kenya alikokulia na kutengeneza nyimbo nyingi zikiwemo ‘hey baby’ ft. Marya na Mtaani.com ft. Avril ambapo this time yuko kwenye headlines na hii video yake mpya ya Dodoma Singida.
Kwenye Interview na millardayo.com Mustafa amethibitisha kwamba video yake mpya imefungiwa kuonyeshwa kwenye vituo vya TV kutokana na warembo walioonekana ndani yake, yani kutokana na mavazi waliyovaa na kujiachia.
Mustafa amesema hajajutia uamuzi wa kuifanya hiyo video na sio kitu kibaya kwake, mbona za kina Nicki Minaj zilizowazi kuliko hizi zinapigwa na vituo hivyohivyo vya TV Kenya? hii inakuwa sio video ya kwanza kutangazwa kutoonyeshwa kwenye TV, zilizotangulia ni ‘nishike’ ya Sauti Sol na You guy ya ‘P unit’
Friday, June 26, 2015
Mashine ya BVR yaibiwa Mwanza, wawili mbaroni
Watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana, waliiba mashine moja inayotumika kwa ajili ya kuandikishia vitambulisho katika daftari la kudumu la wapiga kura (BVR) katika kata ya Kayenze wilayani Magu mkoa wa Mwanza.
Akizungumza na Ea Radio leo, kamanda wa polisi wa mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo, amesema mashine hiyo pamoja na nyingine 13, zilienda kuchajiwa katika nyumba ya kulala wageni ya BM Lodgei, lakini asubuhi zilipofuatwa haikuweza kupatikana.
Kamanda Mkumbo amesema baada ya kupata taarifa ya kuibiwa mashine hiyo, msako mkali ulifanyika ukiwamo wa kuwahoji wasimamizi wa mashine hizo.
Anasema baada ya kufanyika msako mkali kwa kuweka vizuizi sehemu mbalimbali, walifanikiwa kuikuta ikiwa imetelekezwa njiani ikiwa salama bila kuharibiwa, lakini hakuna mtu aliyeweza kukamatwa.
Hata hivyo, kamanda Mkumbo amesema polisi wamefanikiwa kuwashikilia watu wawili wa nyumba hiyo ya kulala wageni kwa mahojiano ili kufahamu mashine hiyo ilivyoweza kutoweka katika mazingira ya kutatanisha.
Aidha, ametoa wito kwa waandikishaji kuwa makini pale wanapohifadhi mashine hizo ili zisiweze kuharibiwa ama kuibiwa na watu wengine.
Thursday, June 25, 2015
Real Madrid wametoa uamuzi kuhusu kumuuza Sergio Ramos Man United By j.twice
Saa zisizopungua 48 baada ya klabu ya Manchester United kuripotiwa kutuma ofa ya kumsajili beki wa kimataifa wa Spain, Sergio Ramos, klabu yake ya Real Madrid imepokea ofa hiyo na imetoa uamuzi.
Manchester United, juzi walituma ofa ya £35million kwa ajili ya kupata saini ya Ramos na klabu ya Madrid wameipiga chini ofa hiyo.
Madrid walimpa taarifa Ramos juu ya uamuzi wao wakati CEO wa klabu hiyo Jose Angel Sanchez alipokutana na Ramos na wawakilishi wake katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo.
Ramos, 29, aliondoka kwenda mapumzikoni huku akiiambia klabu kwamba anataka kufahamu hatma yake kwenye kikosi cha Madrid kabla timu haijakutana kwa ajili ya kwenda kwenye Pre Season Tour mnamo July 10.
Real, pia, hawataki kumpa mwanzo mgumu kocha wao mpya Rafael Benitez kutokana na mgogoro huu wa Ramos.
Ramos amekasirishwa sana baada ya kuona hapewi thamani anayostahili na ameonyesha kuwa tayari kwenda Old Trafford.
Inafahamika kwamba Ramos anapokea mshahara £4m kwa mwaka ndani ya Bernabeu na anataka kupewa mkataba mpya utakaokuwa na thamani ya £6.5m. United wanatajwa kuwa tayari kumtimizia matakwa yake ya mshahara kwa kumpa ofa ya ya mshahara wa £7.8m ili ahamie Old Trafford.
Baada ya Madrid kukataa ofa hiyo sasa taarifa zinasema klabu hiyo inaandaa ofa mpya na itatumwa hivi karibuni.
Ofa hiyo haitomuhusisha golikipa David De Gea kwa namna yoyote.
Baada ya Mbrazil Firmino, Liverpool sasa kumsajili beki huyu wa kiingereza By j.twice
Baada ya kufanikiwa kufanikisha usajili wa Danny Ings kutoka Burnley na Roberto Firmino kutoka Hoffenheim ya Ujerumani, klabu ya Liverpool sasa inatarajia kukamilisha usajili mchezaji mwingine ndaninya saa chache zijazo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyombo vya habari vya England, Liverpool wamefanikiwa kutuma ofa iliyokubaliwa na Southampton kwa ajili ya kumsaini beki wa kimataifa wa England – Nathaniel Clyne.
Liverpool walituma ofa ya £12.5million kwa ajili ya Clyne, na baada ya Southampton kuikubali sasa kilichobaki ni suala la vipimo vya afya ili mchezaji huyo ajiunge nao.
Clyne ambaye yupo katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake na Southampton kwa sasa yupo mapumzikoni na anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka 5 ikiwa atafuzu vipimo vya afya.
Roberto Firmino baada ya kusaini Liverpool
Mchezaji huyu anakuwa mchezaji wa sita kusajiliwa na Liverpool katika dirisha hili la usajili, akiungana na Firmino aliyetua Anfield kwa ada ya £29m. Wachezaji wengine waliosajiliwa ni James Milner, Adam Bogdan na Charlton’s Joe Gomez
Mtoto auawa kikatili Dar, waandikishaji BVR wafungiwa kituoni na Raia wa Kuwait akamatwa JNIA na kobe hai 173…#MAGAZETINI JUNE25 By J.twice
TANZANIA DAIMA
Mtoto anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka mitano hadi sita ameuwa kikatili jijini Dar es salaam baada ya kubakwa na kasha kunyongwa shingo huku akidaiw akunyofolewa sehemu za siri.
Mwili wa mototo huyo unadaiwa kutelekezwa katika moja ya nyumba iliyokuwa haijaisha na kugunduliwa na kijana aliyekuwa akiokota chupa tupu za maji eneo la tabata kisiwani, Dar es salaam.
Baadhi ya mashuhuda walisema walilaani tukio hilona kusema na ukatili huo ni wa kwanza kutokeo mtaani hapo.
“Sisi tupo jirani na yumba hii na hatujasikia kelele zozote na ndio maana tunasema tukio hili halikufanyika hapa” walisema baadhi ya mashuhuda.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo Christopher Victory alikiri ytokea kwa tukio hilo na ofisi yake ilipokea taarifa hizo juzi na kulazimika kytoa taarifa kituo cha Polisi cha Tabata.
Kamanda wa Polisi Ilala Lukas Mkondya alisema taarifa ya unyama huo itawekwa wazi leo baada ya kupokea ripoti ya daktari.
MWANANCHI
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeifuta kesi ya mauaji ya kukusudia iliyokuwa ikimkabili mfanyabiashara Marijan Abubakar, maarufu kama Papa Msofe na mwenzake, Makongoro Joseph.
Hakimu Mkazi, Renatus Rutta aliifuta kesi hiyo chini ya kifungu cha 91 (1) cha sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.
Aliifuta baada ya Wakili wa Serikali Wankyo Simon, kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini ( DPP) kuonyesha kuwa hana nia ya kuendeleza mashtaka dhidi yao.
Msofe na Makongoro wamesota rumande kwa takriban mwaka mmoja sasa kutokana na kile kinachelezwa ni upelelezi kusubiriwa ukamilike.
Msofe kwa mara ya kwanza alifikishwa kortini Agosti 2012.
Hata hivyo baada ya kuachiwa huru Makongoro aliruhusiwa huku Msofe akifunguliwa kesi nyingine ya kughushi.
Katika kesi hiyo mpya, Msofe anadaiwa kuwa Desemba 23, 2004 katika Wilaya ya Ilala kwa nia ya kudanganya alighushi nyaraka ya kuhamisha haki ya umiliki wa nyumba namba 288 ambayo ni mali ya mfanyabiashara wa madini Onesphory Kituli (kwa sasa marehemu).
Ilidaiwa kuwa Msofe kwa nia ya kudanganya alighushi nyaraka hiyo akionyesha Desemba 13,2004, Kituli alihamisha haki yake ya umiliki wa nyumba hiyo kwake wakati akijua ni uongo.
Mbali na shtaka hilo, Msofe anadaiwa kuwa kati ya Desemba 23,2004 na Machi 30, 2005 akiwa na nia ya kidanganya alitoa nyaraka hizo za uongo kwa Kamishna wa Ardhi kwa lengo la kuhamisha umiliki kutoka kwa Kituli kwenda kwake.
Upande wa mashtaka ulidai mahakamani hapo kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Kesi imeahirishwa hadi Julai 9, 2015 na ametakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja atasaini bondi ya Sh 10 milioni.
MWANANCHI
Baraza la Taifa la Elimu la Ufundi (NACTE) limefuta usajili wa vyuo vitatu na kuvishusha hadhi vingine 16 kutokana na kukiuka masharti ya usajili.
Vyuo vilivyofutiwa usajili ni Dar es Salaam College of Clinical Medicine, Ndatele School of Medical Laboratory Sciences, vinavyohusika na elimu ya tiba, na Institute for Information Technology kinachofundisha elimu ya teknolojia ya habari na mawasiliano (Teknohama).
Akitangaza uamuzi huo jijini hapa jana, kaimu katibu mtendaji wa Nacte, Dk Adolf Rutayuga alisema vyuo hivyo vimeshindwa kurekebisha kasoro ambazo baraza hilo lilizibaini na kuvitaka kufanya marekebisho.
Alisema baraza hilo lilitoa notisi ya siku 30 likivitaka vyuo vyenye upungufu katika usajili na ithibati kutoa maelezo na kufanya marekebisho.
Kaimu mkurugenzi huyo alisema baadhi ya vyuo vilifanya marekebisho kama vilivyoogizwa.
Alitaja makosa yaliyokiukwa kuwa ni kumalizika kwa muda wa usajili, kutoanza mchakato wa kupata uthibitisho wa kufikia viwango vilivyowekwa, kumalizika muda wa ithibati na kutoomba upya usajili pamoja na vyuo kuamua kusitisha mafunzo.
Alisema mbali na vyuo hivyo vitatu vilivyofutiwa usajili, vingine 16 vimezuiwa kusajili wanafunzi au kushushwa hadhi.
Alisema Darmiki College of Educational Studies imezuiwa kusajili wanafunzi baada ya kubainiki kinadahili bila kusajiliwa.
Alivitaja vyuo vilivyoshushwa hadhi kuwa ni Sura Technologies, Institute of Management and Information Technology, Techno Brain, Ministry of Agriculture Training Institute Igurusi, Mbozi School of Nursing, KCMC AMO Ophthalmology School, KCMC AMO Anaesthesia School, Advanced Pediatrics Nursing KCMC.
Vingine ni AMO Training Centre cha Tanga, CATC Sumbawanga, CATC Songea, COTC Maswa, COTC Musoma, Dental Therapists Training Center, Ngudu School of Environmental Health Sciences Kwimba na KCMC AMO General School Moshi.
MWANANCHI
Kazi ya uandikishaji wapigakura imezidi kukumbwa na matatizo baada ya wananchi kuwafgungia waandikishaji ndani ya kituo kutokana na kupata taarifa kuwa muda uliopangwa kwa ajili ya mitaa ya Buhalahala, Kisesa na Moringe umekwisha, huku wakiwa hawajapata nafasi ya kusajiliwa.
Wakati vurugu hizo zikitokea, wananchi wa kata nne za wilayani Bukombe wanahofia kukosa nafasi ya kuandikishwa kutokana na maeneo yao kutoingizwa kwenye mfumo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), huku watu watatu, wakiwamo watoto wawili wilayani Hanang wakikamatwa kutokana na kujiandikisha mara mbili huku wakiwa hawajafikia umri unaotakiwa.
Tukio la Geita limetokea siku chache baada ya mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuwataka wananchi mkoani Kilimanjaro kutoruhusu mashine zinazotumika kuandikishia wapigakura kwa njia ya kielektroniki (BVR) kuondolewa vituoni endapo kuna watu ambao hawajaandikishwa.
Uandikishaji mkoani Geita ulianza Juni 17, mwaka huu kwa kata tatu za Buhalahala, Mwatulole na Kalangalala na muda uliopangwa kumalizika ni juzi. Hali ilikuwa mbaya kwenye kata hizo baada ya wananchi kukaa vituoni hadi usiku wakisubiri kuandikishwa, na walipopata taarifa kuwa kazi hiyo haitaendelea kwa kuwa siku zilizopangwa zimemalizika, walichukua uamuzi huo wa kuzuia waandikishaji hadi watakapoandikisha wote waliokuwa wamesalia.
“Nimekuja hapa nina siku ya tano leo (juzi). Kila nikija sipati nafasi ya kuandikishwa wengine wanakesha vituoni siku ya tano, lakini hawajaandikishwa na leo ndiyo mwisho,” alilalamika mkazi wa Mwatulole, Marwa Ernest.
Mkazi mwingine, Neema Charles alisema:“Mwandikishaji anatuambia macho hayaoni, kwa hiyo sisi tufanyeje, tunataka kitambulisho kwani ndiyo cha msingi mwaka huu.”
Wananchi hao ambao walionekana kuwa na jazba, huku wakitishia kuchoma mashine kama wasingeandikishwa, walidai kuwa shughuli hiyo imetawaliwa na rushwa.
Hali hiyo ilikikumba kituo cha Shule ya Sekondari ya Kalangalala, ambako hadi saa 1:30 usiku mwandishi alishuhudia zaidi ya wananchi 200 wakiwa kituoni wengine wakipigana na kusukumana kila mmoja akitaka kuandikishwa.
“Hapa muda unaisha na leo (juzi) ndiyo mwisho, hatujui hatima yetu, wananchi wengi hatujaandikishwa, tumeshaomba tuongezewe mashine lakini hatusikilizwi zaidi tunashuhudia wenye fedha ndiyo wanaandikishwa,” alisema mkazi wa Kisesa, Mariana Peter.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Hellen Kahindi alikiri kuwapo kwa vurugu hizo na kwamba walikosea kuweka vituo pembezoni mwa mji, jambo lililosababisha wananchi wa mjini kukimbilia maeneo hayo wakihofia kutoandikishwa.
Alisema vurugu hizo zilisababisha magari mawili ya Serikali kuvunjwa vioo, huku waandikishaji wakiponea chupuchupu kutokana na kuwapo na vurugu kubwa eneo la kutokea hadi polisi walipoingilia kati.
MWANANCHI
Kada wa CCM, Elidephonce Bilohe, mkulima anayeomba kupitishwa na chama chake kuwania urais, amesema anatumia usafiri wa mabasi ya umma kuzunguka mikoani kusaka wadhamini.
Wakati Bilohe akitumia usafiri huo, wagombea wenzake wanatumia au walitumia mabasi waliyokodi na kuyafanyia maboresho ndani, magari madogo na ndege kutafuta wadhamini 450 kutoka mikoa 15 inayotakiwa kwa mujibu wa taratibu za CCM.
Bilole alisema ameshafika mikoa tisa ambayo ni Dodoma, Kigoma, Geita, Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Tabora, Morogoro na Dar es Salaam, tangu alipochukua fomu hiyo Juni 9.
“Huko kote nimekuwa nikienda kwa kutumia usafiri wa mabasi ya abiria na daladala. Kwa kweli nimepata ushirikiano mzuri kutoka kwa makatibu wa CCM, nawashukuru sana,” alisema.
Bilohe alisema atakwenda mikoa 15 tu kama inavyotakiwa na chama chake, tofauti na watiania wengine ambao baadhi wamekwenda zaidi ya mikoa 20.
“Kwenda mkoa mmoja natumia siku mbili ama tatu kufika na kupata wadhamini. Gharama ni nyingi sana, lakini kwa kuwa nimeshaamua kuwatumikia Watanzania nitakwenda,”alisema.
Alisema kuwa atazirudisha fomu hizo Juni 30 au Julai Mosi kulingana na ratiba yake ya kukusanya wadhamini.
Jumla ya makada 39 wamejitokeza kuwania nafasi hiyo na Bilohe ndiye mgombea pekee aliye na elimu ndogo ya darasa la saba, tofauti na sheria ya nchi inayotaka mgombea wa nafasi hiyo ya juu kisiasa awe na shahada.
Bilohe ni mmoja wa makada wachache waliojitokeza kuomba ridhaa ya CCM ambao hawajawahi kushika madaraka makubwa serikalini au ya kisiasa.
Katika kinyang’anyiro hicho kuna mawaziri wakuu watatu, mawaziri 12 wa sasa, Jaji Mkuu mstaafu, maofisa wa juu wa Idara ya Usalama wa Taifa, maofisa waandamizi wa Serikali ambao wamestaafu na wabunge.
MWANANCHI
Jeshi la Polisi, Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNAI), linamshikilia, raia wa Kuwait, Hussein Mansoor, kwa kukutwa na kobe hai 173 aliokuwa akiwasafirisha kueleka nchini kwake.
Kaimu Mkurugenzi wa Uwanja wa JNIA, Clemence Jingu alisema abiria huyo mwenye hati ya kusafiria yenye namba 003870237, alikamatwa usiku wa kuamkia jana akijitayarisha kupanda ndege ya Emirates iliyokuwa ikielekea Kuwait kupitia Dubai.
Jingu alisema raia huyo alikamatwa saa tano usiku katika eneo la abiria wanaoondoka, baada ya polisi wa JNIA kwa kushirikiana na maofisa wa Wizara ya Maliasili kufanya ukaguzi na kugundua kobe hao wakiwa wamefichwa kwenye masanduku makubwa mawili.
“Hii ni moja ya kazi kubwa ambazo tunazifanya kwa sasa hapa JNIA, ila tutahakikisha kuwa hakuna nyara za Serikali zitakazotaifishwa na kupitishwa hapa kwa kuwa tumeimarisha ulinzi maradufu,” Jingu.
Jingu alisema kobe hao wenye thamani ya Sh 30 milioni ni miongoni mwa nyara muhimu za Serikali ambazo zimekuwa zikitaifishwa kupitia mbinu mbalimbali.
“Pamoja na kuimarisha ulinzi, lakini tutahakikisha JNIA inakuwa bora kuliko viwanja vingine vya Afrika Mashariki na zaidi hasa kuhakikisha ulinzi unapewa kipaumbele” alisema.
Kamanda wa Polisi wa JNIA, Khamis Suleiman, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa huyo anashikiliwa na jeshi hilo kwa uchunguzi zaidi.
Tukio hilo lilithibitishwa pia na Kamishna wa Interpol, Tawi la Tanzania, Gustav Babile ambaye alisema raia huyo alikamatwa na wanyama hao huku akiwa na vibali halali.
Mmoja wa wafanyakazi wa JNIA alisema kabla ya kukamatwa, ilionekana kuna mpango umefanywa ili kumpitisha raia huyo bila kugundulika kwani taa za eneo la ukaguzi zilizimwa kwa saa kadhaa uwanjani hapo.
“Si kawaida taa kuzimwa lakini wakati yeye anapita taa zilizima jambo linaloonyesha kuwa ni njama zilizopangwa lakini hata hivyo hazikufanikiwa,” kilisema chanzo hicho.
Tukio hili linafanana kwa kiasi kikubwa na lile lililotokea Januari 8, mwaka huu, ambapo raia mwingine wa Kuwait, Ahmed Ally Mansour alikamatwa uwanja wa JNIA akiwatorosha kenge hai 149 wenye thamani ya Sh 6.3 milioni.
NIPASHE
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya Arumeru na Diwani wa kata ya Mlangarini wilayani humo, Mathias Manga, amenusurika kuuawa baada ya watu wasiojulikana waliokuwa wakimfuatilia kumpiga risasi nje ya geti la nyumba yake
Manga ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu wa Tanzanite huko Mirerani, mkoani humu ni mmoja kati ya marafiki wakubwa wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ambaye ametangaza nia ya kuomba ridhaa ya CCM kumteua kuwa mgombea wa kiti cha urais katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
Manga alikuwa Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kumtafutia wadhamini Lowassa mkoani Arusha, kazi ambayo ilikamilika jana baada ya kupata wadhamini 12o,339.
Haijafahamika rasmi iwapo tukio la kupigwa risasi na kujeruhiwa kwake, lina uhusiano wowote wa kibiashara au kisiasa, kwa sababu Manga mwenyewe hakutaka kuzungumza na waandishi wa habari kuhusiana na suala hilo.
Awali alisema angezungumza na waandishi wa habari baada ya nusu saa kwa vile alikuwa katika mazingira ambayo hayakuwa mazuri kuzungumza, lakini alipopigiwa tena simu alisema hawezi kuzungumza chochote.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo eneo la Ngarenaro na risasi hiyo ilimparaza Manga maeneo ya ubavu wa kulia.
“Alitoka katika shughuli zake za kawaida na alipokuwa anarejea nyumbani kwake eneo la Ngarenaro kwenye nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa, ghafla aliona gari likimfuata kwa nyuma na alipokuwa akitembea kwa kasi nalo liliongeza mwendo, akahisi watu hao wanamfuata, hivyo akazidi kuongeza mwendo hadi alipofika getini kwake na lile gari pia lilieggeshwa kwa nyuma yake,” alisema.
Alisema kwa maelezo ya Manga watu hao walikuwa watano na wote walikimbia bila kuchukua kitu chochote na yeye alipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru kwa matibabu ambako alipata matibabu na kuruhusiwa kurudi nyumbani kutokana na kutoumia sana.
Lowassa jana wakati wa kudhaminiwa mkoani Arusha jana, alimpa pole Manga kutokana na tukio hilo kinalidaiwa kufanywa na majambazi.
NIPASHE
Bunge limesikia maoni ya wadau ya kuuondoa Bungeni Muswada wa Sheria ya Haki ya Kupata Habari 2015 ambao ulitarajiwa kusomwa kwa mara ya pili Juni 27, mwaka huu.
Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, alithibitisha hayo jana kwenye viwanja vya Bunge wakati akihojiwa kutaka kujua iwapo ushauri wa kamati umemfikia Spika na uamuzi juu ya suala hilo.
“Ushauri wa kamati umezingatiwa, Muswada umeondolewa Bungeni,” Dk. Kashilillah.
Aidha, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, alisisitiza kuwa maoni ya wadau hayawezi kupuuzwa katika uandaaji wa Muswada wa Sheria ya Haki ya Kupata Habari, 2015.
“Hatutapuuza maoni ya wadau hasa yanayolenga kuboresha muswada husika. Utungaji wa sheria yoyote ni lazima uwe shirikishi, hivyo maoni ya wadau yamesikikizwa kama ilivyokuwa awali walishauri Muswada huo na ule wa Huduma kwa Vyombo vya Habari, usije kwa hati ya dharura, tulizingatia na uliondolewa,” alibainisha.
Juni 22, mwaka huu, wadau mbalimbali wa habari waliokutana jijini Dar es Salaam, walipinga miswada hiyo kwa kile kinachoelezwa kuwa inakiuka sheria za kimataifa, Katiba ya nchi na kuwanyima haki raia kupata taarifa na kuua ndoto ya vijana wanaotarajia kunufaika na tasnia ya habari.
Wadau hao ni Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania ( MOAT), Baraza la Habari Tanzania (MCT), Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) Tawi la Tanzania na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu ( THRDC).
Mmiliki wa Kampuni ya New Habari Corperation, Rostam Aziz, alisema muswada huo ni mbaya kwani unazuia dhana nzima ya uwazi na ukweli hivyo kulirudisha taifa nyuma na kuitaka serikali kutopeleka bungeni hadi wadau wote wa tasnia ya habari watakapotoa maoni.
“Serikali isifanye haraka, muswada huu utaturudisha nyuma kama taifa. Usitishwe kupelekwa bungeni hadi pale wadau wote watakapotoa maoni yao,” Rostam.
Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga, alisema baraza hilo limetoa ombi hilo kwa sababu wadau wa habari hawakuwa na muda wa kutosha kutoa maoni yao baada ya kusomwa kwa mara ya kwanza wiki iliyopita.
HABARILEO
Rais Jakaya Kikwete amewashangaa wanasiasa wanaokosoa kitendo cha Serikali yake kukopa fedha nje ya nchi kuwa kinazidisha deni la taifa, kwamba hawana ufahamu na kufafanua kuwa katika kuharakisha maendeleo ya nchi, kukopa ni jambo la kawaida.
Alisema hata mataifa makubwa yaliyopiga hatua kubwa kwenye maendeleo yamekuwa yanakopa na akasisitiza kuwa uamuzi wa serikali kwenda nje kukopa amekuwa anaufanya ili kupata fedha kwa ajili ya kujenga miundombinu ambayo itaifanya nchi ipige hatua kubwa kimaendeleo.
Alitoa mfano kuwa hata kama mtu anaendesha duka ni lazima akakope benki kama anataka kuendeleza duka lake, kama hatafanya hivyo kwa kuamini kuwa fedha anazopata kwa kuuza bidhaa zitalitunisha duka hilo basi asubiri miujiza ya kumpatia faida.
Aliyasema hayo wakati akizungumzia uamuzi wa serikali yake kuwenda kukopa nje kwa ajili ya kujenga miundombinu mbalimbali, ikiwemo ujenzi wa mkongo wa taifa ambao alisema lengo lake ni kuweka misingi ya miundombinu wakati taifa linapoelekea kwenye utekelezaji wa ujenzi wa viwanda vya kisasa.
Rais Kikwete alisema baada ya kufanya uamuzi huo aliamua pia kuwekeza kwenye utafiti kwa kuhakikisha kuwa Serikal inatenga fedha kwa ajili ya kuwasomesha watafiti, kununua vifaa vya utafiti na kukarabati vituo vya utafiti ambayo alisema vingi vilikuwa kwenye hali mbaya.
“Tulianza na Sh bilioni 10, tunashukuru sasa hivi tupo kwenye Sh bilioni 60 na naamini kuwa Rais atakayekuja ataendeleze juhudi hizi kwa kutenga fedha zaidi kwa ajili ya tafiti maana nikiangalia hali ya baadaye ya maendeleo ya nchi hii inategemea watafiti, wanasayansi na wabunifu,” Rais Kikwete.
Rais alisema anajivuna kwamba anaondoka madarakani wakati shughuli za utafiti zimepata uhai na kwamba juhudi zilizofanywa na Serikali yake za kuwaendeleza wabunifu zimezaa matunda mengi kwani kwa sasa nchi ina watafiti wazee na vijana wanaofanya mambo makubwa yanayotambulika kimataifa.
Alisema fedha zilizotolewa na serikali yake zimesaidia kusomesha watafiti 517 katika kozi za shahada ya uzamili na uzamivu na vituo 20 vimekarabatiwa na miradi 70 ya utafiti imetekelezwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Dk Hassan Mshinda alisema kongamano hilo la nne limewakusanya wanasayansi, watafiti, watunga sera na wabunifu mbalimbali.
Alisema mada 80 zitajadiliwa ikiwemo tafiti mbalimbali zilizofanywa na watafiti wa ndani, kujadiliana changamoto za kupeleka utafiti sokoni na upatikanaji wa teknolojia na jinsi ya kuhuisha sayansi asili na sayansi ya kisasa.

Linah kwenye studio ya Millard Ayo! ishu ya boyfriend wake na Wema Sepetu kaizungumzia hapa By j.twice
Linah ni mwimbaji wa bongofleva ambapo hivi karibuni mpaka Mama yake mzazi alimpigia simu kutaka ajiepushe kugombana na watu baada ya kusikia stori kwamba anagombea Mwanaume na Wema Sepetu.
Ilimfanya mama afikie hatua hiyo baada ya kusikia tu stori za watu na baadhi ya mitandao na gazeti lililoandika hiyo habari lakini ukweli wenyewe kutoka kwa Linah uko kwenye hii video ya Interview aliyofanyiwa TZA kwenye studio ya Millard Ayo.
Linah ni mwimbaji wa bongofleva ambapo hivi karibuni mpaka Mama yake mzazi alimpigia simu kutaka ajiepushe kugombana na watu baada ya kusikia stori kwamba anagombea Mwanaume na Wema Sepetu.
Malaika wa Uswazi Take Away katuletea hii video mpya ya ‘SARE’ Ft. Mesen Selekta By j.twice
Ni miongoni mwa waimbaji wazuri wa kike Tanzania wenye mvuto kuanzia kwenye sauti zao na swagg zao ambapo kama damu yako inachembechembe nyingi za bongofleva, sauti yake utakua uliisikia kwenye hit single ya USWAZI TAKE AWAY aliyoshirikishwa na Chege.
Sasa hivi Malaika huyu anazo headlines za single zake peke yake ambapo video yake mpya inaitwa Sare na unaweza kuitazama hapa.
Ni miongoni mwa waimbaji wazuri wa kike Tanzania wenye mvuto kuanzia kwenye sauti zao na swagg zao ambapo kama damu yako inachembechembe nyingi za bongofleva, sauti yake utakua uliisikia kwenye hit single ya USWAZI TAKE AWAY aliyoshirikishwa na Chege.
Wednesday, June 24, 2015
Ishu ya Banza Stone kuzushiwa kifo kayazungumza haya stori kamili iko hapa By j.twice
.
Baada ya kuzushiwa kifo ,muimbaji mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Banza Stone amesema si jambo la busara la kuzushiana kifo
Alisema ‘Mimi nilikuwa nasumbuliwa na kinjwa sana na ki homa homa fulani kama miezi miwili lakini saaa hivi niko vizuri, naelendele poa na leo nilienda hospitali daktari kufanya sound check akaniambia kuwa malaria
TZA:…’Jana ilikua ni mara ngapi kuzushiwa kifo ?
Banza Stone:..’Mimi hata sijui ila nasikia mara watu oooh banza kafaa, mara ooh kila mtu anaongea lake ila mimi niko poa ni mzima naweza kufanya kazi ila kwasasa siko tayari kufanya kazi kwani nitauchosha mwili mwangu
TZA:Vipi kuhusu kazi zako za muziki bado unaendelea nazo ama au ??
Banza Stone’…..Naweza kusema ninaendelea na muziki kama kawaida kwasababu sasa hivi nina kama nyimbo sita mpya ziko ndani kesho, kesho kutwa naweza nikaamua niachie moja mpaka video ziko tayari sio za bendi bali ni zangu binafsi…’
Cheki Mpira utakaotumiwa kwenye ligi ya England msimu ujao. By j.twice
Kukiwa kumesalia mizi miwili na siku kadhaa kabla ya ligi kuu ya England na lingi nyingine kubwa barani ulaya kuanza mpira rasmi utakaotumika kwenye ligi ya England umefahamika .
Mpira huo umebuniwa na kampuni ya vifaa vya michezo ya Kimarekani ya Nike ambapo utakuwa unafahamika kwa jina la Nike Ordem na umetengenezwa kwa kuzingatia teknolojia ya kisasa ambayo inaendana na mabadiliko ya mchezo wa soka .
Mpira huo umetengenezwa kwa kuzingatia jinsi ambavyo wachezaji watakuwa wakiutumia uwanjani ambapo moja ya vitu vilivyozingatiwa ni rangi yake na umetengenezwa kwa rangi angavu ili kuwasaidia wachezaji kuuona wakiwa uwanjani na kufanya maamuzi ya haraka.
Beki wa West Ham United James Tomkins akiwa anaujaribu mpira mpya ambao utatumika kwenye msimu ujao wa ligi ya England .
Mpira huo pia una sehemu 12 ambazo zinaufunika ili kuusaidia kwenda na kasi ambayo itawasaidia wachezaji wenye uwezo wa kupiga mashuti ya mbali .
Mpira huo ambao unatarajiwa kuzinduliwa mwezi julai pia utatumika kwenye ligi za Hispania na Italia na umeonekana ukifanyiwa majaribio na wachezaji wa klabu ya West Ham United kwenye uwanja wao wa mazoezi .
Winga wa West Ham Matt Jarvis akionekana akijaribu mpira huu ambao pia utatumika kwenye ligi za Hispania na Italia .
Tuesday, June 23, 2015
P Diddy matatani, ajikuta mikononi mwa polisi!! By j.twice
Multi-millionea na HipHop superstar P Diddy ameingia kwenye headlines za leo baada ya kujikuta matatani na polisi kwa kosa la kumshambulia kocha wa mpira katika mazoezi ya mechi ya mpira ya mwanae katika chuo cha UCLA.
Msanii huyo alikamatwa kwenye majira ya saa sita na nusu mchana kwenye maeneo ya Acosta Athletic Training Complex, na kufunguliwa file la makosa hayo, japo hakuna mtu yoyote aliumia P Diddy aliweka selo kuanzia saa sita hadi saa kumi na mbili na kuachiliwa baada ya kushindwa kupata kisa kamili cha kwa nini shambulio hilo lilitokea.
Lakini licha ya P Diddy kuachiliwa, polisi wamesma milionea huyo alitakiwa kufikishwa jijini Los Angeles kwenye County Sheriff’s Department Inmate Reception Center na bado mipango hio inaendelea.

Jose Chameleone karudi tena kwenye headlines na Video hii ‘Bwerere’ By J.twice
Staa wa East Afrika Jose Chameleone amerudi kwenye headlines kwa mara nyingine na safari hii ameachia Video ya nyimbo yake mpaya ya inayoitwa ‘Bwerere’.
Katika video hiyo iliyofanyika Uganda imefanyika chini ya mtayarishaji Nolton pamoja na George.
Itazame hapa mtu wangu…

Maamuzi ya Mahakama kuhusu kesi aliyoifungua Mbunge Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ dhidi ya mkewe wa zamani By j.twice
Ni habari ambayo imeandikwa na gazeti ya Mwananchi June 23 2015 ikitokea Mahakamani Manzese Dar es salaam kuhusu kesi iliyokua imefunguliwa na Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi kuhusu mke wake wa zamani.
Taarifa inasema Mahakama ya Manzese imeamuru Mbunge Joseph Mbilinyi akabidhiwe mtoto wao kutokana na kesi aliyoifungua dhidi ya mke wake huyu akidai anamuharibu mtoto.
Hii habari imekuja siku kadhaa tu baada ya TUZO ZA KILI 2015 ambapo mke huyu wa zamani aliingia kwenye headlines kutokana na vazi alilokuwa amevaa.

Mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2008 kuisikia album ya staa wa muziki Janeth Jackson ambaye ni moja ya watoto mastaa kutoka kwenye familia ya mzee Joseph Walter “Joe” Jackson.. Familia yao yote iko kwenye Entertainment Industry, lakini kwa miaka saba Janeth hajawahi kuachia album wala single yoyote !!
Ujio wake mwingine rasmi kabisa ni huu ndani ya 2015, kaachia hii single inayoitwa ‘No Sleep‘, nimeisogeza hapa uisikilize alafu utaniambia kwenye comment yako kama huu ujio unaounaje !!
Drake na nickminaj wabwagamanyanga cash money by j.twice
Msanii na mmoja kati ya watu wanaounda team ya Cash Money Records Lil Wayne aliingia kwenye headlines kipindi cha nyuma kwa madai ya kutaka kutoka katika label hio ya muziki. Headlines mpya leo ni kwamba msanii huyo wa Hiphop amefungua kesi mahakamani dhidi ya Cash Money kwa madai ya kwamba eti Nicki Minaj na Drake hawana usimamizi mzuri chini ya lebo hio.
So ina maanisha Nicki Minaj na Drake wako njiani kuimwaga Cash Money Records? ama ni stori tu!?
Katika documents zilizowasilishwa mahakamani Lil Wayne amedai kua sio yeye peke yake anae wadai lebo ya hio ya muziki bali lebo hio imeendelea kukataa kuwalipa wasanii wengine chini ya lebo hio pesa zao, na kusisitiza kua visa hivi vitasababisha yeye na baadhi ya wasanii aliowaleta kwenye lebo hio kutemana na Cash Money Records.
Msaani huyu alieibua vipaji vya Drake, Nicki Minaj na J.Prince amedai kua Birdman alimuahidi asilimia kubwa ya pesa ya Cash Money Records kutoka kwenye faida ya kumgundua Drake alieiingizia lebo hio faida zaidi ya dola millioni 40 lakini akashangaa jamaa amemlipa millioni mbili tu kati ya mamilioni aliotakiwa kulipwa.

Monday, June 22, 2015
Kala Jeremiah kayasema haya kuhusu viongozi wanaotangaza nia 2015. By j.twicee
Baada ya makada mbalimbali kutangaza nia na hatimaye kuchukua fomu za kugombea urais, Rapper Kala Jeremiah amefunguka na kuwataka wananchi wote kuchagua kiongozi sahihi mwenye sifa za kuingoza nchi.
‘Tumchague mtu na tusishawishike na vyama, tumchague mtu ambaye tuna mwamini, Tanzania imefika sehemu ambayo sio sehemu nzuri sana kwa maana ya kwamba tumekuwa tunaahidiwa vitu vingi sana mwisho wa siku bado wananchi wanalalamika lakini pia kumekuwa na mikataba mingi ambayo hata wananchi hawaijui kwa hiyo mtu anaposaini mkataba tulikuwa tunaomba wananchi waipitie kwanza tuangalie faida za kiongozi
Kwa hiyo naomba vijana wenzangu tusishawishe kisiasa tuangalie mtu ambaye ana uwezo wa kuamua jambo sio tu kwasababu tumesikia ameongea vizuri hapana tuangalie pia nyuma alishawahi kufanya kazi ipi ambayo alitekeleza kwenye jamii, naamini safari hii wananchi wamtachagua kiongozi atakayekuwa na misimamo sahihi ya kuwajibisha watu moja kwa moja bila kuangalia usoni.

Unajua watoto waongo wana kitu gani kizuri? Wataalam wamekuja na hili jibu !! By j.twice
Kuna upande mwingine eti uongo ni kitu kizuri?? Wataalam wa Saikolojia Uingereza wamekuja na Ripoti yao nyingine mtu wangu.. eti ni kweli watoto wadogo ambao ni waongo wana uwezo mzuri wa kutunza kumbukumbu?
Wataalam waliwachukua watoto wenye umri kati ya miaka sita na saba na kuwafanyia majaribio ya kucheza game, baadae walipoulizwa kuhusu walivyocheza game majibu ikaonekana watoto ambao waliongea uongo wana uwezo mkubwa zaidi wa kutunza kumbukumbu kwa vile wanakumbuka kila kitu kuanzia cha uongo na cha ukweli walichokifanya!!
Una mtoto ambae ana tabia ya kuongopa? Kama akikudanganya basi ujue ana hii sifa nyingine nzuri mtu wangu !!
SIASA South Africa kwenye headlines na vurugu alizofanyiwa Rais Jacob Zuma bungeni!! By j.twice
Tarehe 19 June mwaka huu Bunge la South Africa liliingia kwenye headlines katika vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii baada ya baadhi ya viongozi kutoka chama cha upinzani kuanzisha vurugu zilizo pelekea kuahirishwa kwa Bunge hilo siku ya ijumaa.
Bunge la South Africa liliingia vurugu baada ya wanachama wa Economic Freedom Fighters kumzuia Rais Jacob Zuma kuendelea kutoa ripoti aliokusudia kuwasilisha mbele ya Bunge hilo kwa kumshambulia Rais huyo na maswali yanayohsu uwajibikaji wake, maswali ambayo yaliongaishwa na malalamiko ya yeye kukiuka Katiba ya nchi hiyo, kitendo kilichopelekea Rais huyo kutokupewa nafasi ya kujieleza.
Kitendo hichi kilimlazimu Spika wa bunge Baleka Mbete kuahirisha Bunge hilo na kuita kikao cha dharula na vyama hivyo nje ya Bunge hilo baada ya vurugu kutapakaa Bungeni hapo, na alipohojiwa na vyombo vya habari, Spika wa Bunge la South Africa alisema amesikitishwa na kitendo hiki kufanyika na baadhi ya watu wanaotazamwa na jamii kama viongozi, na kuongeza kua, kitendo hicho sio mara ya kwanza kutokea… iliwahi kutokea mwezi Agosti tarehe 21 mwaka jana ambako pia alilazimika kuahirisha Bunge hilo kutokana na vurugu kuanzishwa na vyama vya upinzani.
Bunge la South Africa limepinga baadhi ya malalamiko kutoka kwa viongozi wa vyama vya upinzani kua Rais Jacob Zuma anakiuka Katiba na kuepuka uwajibikaji na kusema kua Rais huyo anategema kuonekana tena Bungeni mwezi Agosti mwaka huu kwa ajili ya kutoa ripoti hio kama Sheria ya nchi inavyomtaka kufanya hivyo mara nne kwa mwaka na mara moja kwa mwaka katika Baraza la taifa la majimbo.
Hali ilivyo baada ya Bunge kuvamiwa Pakistan leo June 22 2015 by j.twice
Hali sio nzuri Pakistan, kingine kilichochukua headlines kwenye TV za Kimataifa na Mitandaoni ni ishu ya kuvamiwa kwa Bunge la nchi hiyo, mabomu na risasi vimetumika pia !!
Wavamiaji hawakuwa nna nia njema, ripoti zinaonesha jamaa hao walikuwa sita na ni members wa Kundi la Taliban.
Polisi wamefanikiwa kuwaua jamaa hao ambao walikuwa na silaha pamoja na mabomu, hapa ninazo pichaz ambazo zinaonesha jengo la Bunge kwa ndani likiwa na moshi mzito
Wavamiaji hao walilipua gari moja nje ya Jengo la Bunge kabla ya kuvamia ndani !! Watu 18 wameumia kwenye tukio hilo.

GENERAL NEWS Unyama huu wa baba kwa binti yake na utetezi wake mahakamani.. By J.twice
Si jambo la kawaida mzazi kuwa na uhusiano na mtoto wake wa kumzaa, na jamii nyingi zimekuwa zikipinga na kukemea maovu ambayo hufanywa na baadhi ya wazazi kuwafanyia vitendo ya unyanyasaji watoto wao hasa wale ambao hata hufikia hatua ya kubaka binti zao.
Kuna hii imetokea kule Zimbwabwe baada ya baba kumbaka binti yake wa miaka 15 kisha kumwambia ni utaratibu wa utamaduni wao kutembea na mtoto wa kwanza ndani ya familia.
Hata hivyo polisi hawakumuachia baba huyo baada ya kumfungulia mashtaka kwa kosa la ubakaji baada ya tukio hilo la aibu lakini aliendelea kujitetea kuwa ni utamaduni wa jamii yao.
Kwa mujibu wa muendesha mashtaka Mufaro Mageza alisema binti huyo alikwenda kumsalimia baba yake baada ya wazazi wake kutengana na siku ya tatu tangu afike nyumbani hapo baba yake alirudi nyumbani na kwenda moja kwa moja kwenye chumba cha mtoto huyo kisha kumbaka.

Wema Sepetu kuhusu mtoto na Diamond, ujauzito wa Zari na mimba aliyotoa. ( video ) By j.twice
Mahojiano na mwigizaji Wema Sepetu kwenye TV show ya TAKE ONE CloudsTV na Zamaradi Mketema yalimalizika kwa hiki kipisi cha dakika 15 Wema akielezea mengi ya moyoni ikiwemo ya kupata mtoto na Diamond, Ujauzito wa Zari na mimba aliyowahi kuitoa.
Millard Ayo kahojiwa na Sporah kuhusu maisha yake, kazi na alipotokea. (video) By j.twice
Mtu wako wa nguvu Millard Ayo alipata nafasi ya kualikwa na kuhojiwa na mtangazaji Mtanzania Sporah kutoka kwenye THE SPORAH SHOW, show ya TV ambayo kwa muda mrefu imefanya kazi nzuri ya kuhoji watu mbalimbali.
Sunday, June 21, 2015
» Wamembaka Mke Wangu, Nimeona Niachane Nae tu'.....Soma Stori hii Utajifunza Kitu
Ndoa yangu sasa ina miaka 8, tuna watoto 3 na tumejenga nyumba mbili, wiki mbili zilizopita mke wangu alibakwa na watu wawili waliokua wamejenga nae ukaribu kwa lengo la kumhadaa. Siku ya tukio alipigiwa simu na hao jamaa kwamba kuna shamba limepatikana Bagamoyo hivyo wakaliangalie sikuwahi kujua kama anahitaji shamba.Ilikuwa ni Jumapili asubuhi akaniacha home nimepumzika akaenda ili alione hilo shamba.
Hatukuwasiliana tena hadi saa nne usiku nilipotaka kujua mwenzangu yuko wapi simu iliita tu bila kupokelewa, nilishtuka kwa kweli maana hana tabia ya kutonipokelea simu, baada ya muda ikawa haipatikani, nikaanza kumpigia kwa namba yake ya Tigo ambayo iliita tu bila kupokelewa, ilipofika saa sita usiku nikampigia mama yake mzazi nae anasema kwa siku hiyo hajafika pale nyumbani.
Tukapeana jukumu la kuendelea kumtafuta hewani ingawa sio mara ya kwanza kurudi home mida hiyo, wakati mwingine anakuja mida hiyo anadai anatoka Kitchen Party na kadi anakuwa nayo kweli, nikimuuliza kwanini hakuomba ruhusa anajibu ""ningekuomba ungenikatalia"."
Hivyo nikajipa moyo kuwa huenda ameenda kwenye Kitchen Party kama siku zingine nikaendelea kusubiri, hadi saa nane usiku wapi hajaonekana, na bahati mbaya hakwenda na Gari lake siku hiyo lilikuwa na matatizo kwenye injini lilikuwa likisumbua wiki yote hiyo, nikaamua kwenda kwao usiku huo huo, nikamwambia housegirl kuwa mama akija sipo mnipigie ila mkae macho yenu yakiwa getini maana Leo hana Gari.
Tukiwa kwao tayari ilikuwa saa Tisa usiku tukashauriana kwenda Muhimbili baada ya kushauriwa na binamu wa wife aliepigiwa simu na mama mkwe usiku huo. Kwa upande wa majeruhi hakuwepo, nikapelekwa walipozipanga maiti zilizoingia usiku huo na ambazo hazijaenda mochwari sikufanikiwa, mama mkwe aliogopa kuzitazama.
Saa kumi na mbili asubuhi nikamrudisha mama mkwe kwake nami nikaa hapo hadi saa tatu nilipoona simu ya wife ya Tigo ikiita nikapokea, ni sauti ya kike ya mtu mwingine mwanamke. Kumbe wale jamaa wawili walimwekea dawa za kulevya wife kwenye soda hivyo akazimika na kuchukua chumba Gesti na kumwingiza humo, asubuhi tukaenda na ndugu kwa wife na mama mkwe baada ya kupokea hiyo simu ya binti wa mapokezi ambae alitumia simu ya wife ya kitochi waliyomwachia kitandani na kunipigia baada ya kukuta jina la hubby.
Tulipofika tulienda kwenye Chumba hicho tulikuta wife anakoroma na kutoa udenda wenye damu kwa mbali, pembeni yake kulikuwa na kondomu zilizotumika na kinyesi kiasi, mama yake alianza kulia kwa sauti.Kaka yake akampa kibano kikali receptionist aseme ukweli lakini binti wa watu akasema hajui chochote kuna watu wawili waliingia wamembeba na kulipia, na wakatoka asubuhi na mapema.
Anyway, kwa kifupi ni kwamba alitibiwa, alikaa hospital siku tano akipewa dripu na dawa za kuondoa sumu mwilini, hadi hali yake ikawa sawa, kwa ushirikiano alioutoa kwa polisi, na kwa kutumia TCRA ambao wana wapelelezi wao wanaoshirikiana na CID madalali wale walikamatwa wote wawili, mhudumu Wa gesti akaunganishwa kwenye kesi hiyo ya ubakaji ingawa yeye mashtaka yake yanasomeka tofauti na wenzie.
Wamepandishwa kizimbani mara moja na kesi yao kutajwa na imeahirishwa, wapo Segerea, sijajua walishindwa masharti ya dhamana au nini kilitokea maana mimi nilijitoa kwenye kesi hiyo nimewaacha ndugu waendelee nayo, nina sababu.
Tulikotoka na mwanamke huyu:-
Kiukweli Haya yaliyompata ni matokeo ya kunidharau na kutoniheshimu kama mumewe, amekuwa mtu wa ratiba masaa 24/7 per week, anachoamua anakifanya bila consultation na Mimi, mfano:-Aliamua kujiunga na masomo ya jioni baada ya kazi kama ifuatavyo. Alijiunga na diploma ya IT ucc inayoanza saa 11 jioni hadi saa moja jioni, hapo hapo akajiunga na masters ya MBA inayoanza saa moja na kuisha saa nane usiku usiku hadi kufika home ni saa tano na kitu nikamuuliza familia yako nani atai attend? Majukumu yako nani atayafanya? Akanijibu ndio hivyo nimeshajiunga, hakuwa na sababu ya kujiunga na IT angeanza na masters (prioritizing)
Wakuu, mambo yake yote ni siri hasemi mipango yake, anajifanya mtu wa madili anadili na wanaume kuhusu biashara mbali mbali bila kunishirikisha ingawa ni muajiriwa. Mama yake ndio msiri wake mkubwa.
Akienda kokote atoi taarifa hadi akifika huko ndio anasema "" hny nipo kwenye send off"".Nikajaribu kutafuta huenda ana mwanaume nje lakini kiukweli upepelezi na intelligence iliyotukuka ilithibitisha pasipo na shaka kuwa hajawahi Ku cheat.
Simu zake zote niliwahi kuziweka under 24 hrs surveillance kupitia watu wangu wanaofanya kwenye mitando ya simu lakini mawasiliaƱo yote na wanaume ni ya kikazi na madili mbalimbali. Pia niliwahi ku hack namba za simu na account za kijamii zote pia nilitoka bila bila. Lakini hata bedroom life ni nzuri tu, maana ukishindwa kumshika mke kwingineko basi utamshika kwenye haki ya ndoa, mwanamke hawezi kutumikia wanaume wawili kusionekane kasoro,lakini hata upande huo kwa kweli hakuna tatizo.
Sababu niliyoigundua ni mali alizoachiwa na marehemu baba yake ambazo wamepewa mirathi kama miaka minne iliyopita, wapo watatu, baba yao aliacha plot na nyumba nyingi kwenye prime areas hivyo mke wangu amepewa sehemu nyingi anazochukua kodi kubwa sana achilia mbali sehemu alizouza. Hivyo ni mkakati wake na mama yake anifiche vitu vingi ili nisije kumdhulumu anaona ni bora ashirikiane na mama yake kwenye mambo yake.
Hati zangu anajua zilipo in case nimeanguka ghafla ila za kwake zote alizopewa plot zaidi ya 6 ambazo tayari amebadilisha tayari majina kuja ya kwake kazificha nisipopajua nimeshachoka, nashukuru Mungu hili tatizo la kubakwa na kulawitiwa limetokea nimepata pa kumwachia, nasubiri awe vizuri psychologically nianze mchakato wa talaka. Naomba muelewe sikuja hapa kuomba ushauri bali kuwapa funzo wa akina dada na wengine.
Maana nilimwambia hivi. """ hizi mbio zote unazokwenda resi ipo siku watanipigia simu nikufuate Mochwari au Muhimbili"". Na kweli imetokea. Sina haja na pesa zake nina zangu nazopata kazini nilizofanyia maendeleo makubwa tu na miradi kadhaa.Wanashangaa kwanini sijihusishi na hiyo kesi, ni kwa sababu nilimuonya mtoto kwao hakusikia na akanidharau, tried to be a man and more than a man lakini ndo tunazidi kuvurugana. Maana kuna watakaokimbilia kudai "" act like a man"" humu Jf as walikuwa wanaona I am not acting like one.
Mungu akikupa mke wa ovyo hata uki act like Tyson haitasaidia kitu. Sasahivi wamerundikana hapo nyumbani mara leo wamletee pastor, kesho wamletee counselor, mimi jioni naenda zangu kwenye bia narudi nipo vizuri nalala.Juzi alikuja mshauri nasaha kuniambia ameniletea habari njema vipimo vimeonesha wife hana HIV so natakiwa nifurahi.
Nikamjibu mwambie afurahi mwenye matokeo mwenyewe mimi sitaendelea nae, sasa sijui amewaambia, maana mama mkwe ananiangalia jicho kama vile anamwangalia shetani.
Anyway nadhani nimepona rohoni kwa kuwaambia habari hii , sihitaji ushauri, nina maamuzi tayari. Huenda victim mwenyewe akipata mme mwingine atabadilika.
By j.twice

Subscribe to:
Comments (Atom)