Wednesday, June 17, 2015
AJALI Arturo Vidal wa Juventus kapata ajali.. pamoja na hayo kaingia kwenye matatizo! By j.twice
Nyota huyu anatarajiwa kupandishwa Mahakamani hivi karibuni kujibu mashtaka ya kuendesha gari akiwa ametumia kilevi na tayari amenyang’anywa leseni yake.
Kiungo wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Chile, Arturo Vidal amekutwa na huu mkasa ambao huenda atapenda kuusahau haraka iwezekanavyo wakati akiwa na timu yake ya taifa ambayo kwa mwaka huu imekuwa mwenyeji wa michuano ya Copa America.
Vidal ambaye amekuwa kwenye kiwango bora tangu kuanza kwa michuano hiyo akiwa amefunga mabao matatu kwenye mechi mbili amehusika kwenye ajali ya gari ambayo imeelezwa kuwa yeye mwenyewe ndio alikuwa chanzo cha ajali
Ripoti ya Polisi inaonesha kuwa Vidal alikuwa amelewa wakati akiwa anaendesha gari aina ya Ferarri na alisababisha ajali ambayo ilimsababishia majeraha madogo pamoja na mkewe ambae nae alikuwemo ndani ya gari hiyo.
Wote wawili waliwahishwa hospitalini ambako wamekuwa wakitibiwa huku hali zao zikielezwa kuwa sio mbaya kutokana na kupata majeraha madogo kwenye ajali
Vidal alikuwa akitoka kwenye klabu moja ya usiku baada ya wachezaji wa Chile kupewa ruhusu ya kuondoka kambini baada ya mchezo wao dhidi ya Mexico.
Ripoti zaidi zinasema kuwa Vidal huenda akafukuzwa kambini ikiwa ni moja ya hatua za kinidhamu toka kwa kocha wa timu ya taifa ya Chile, Jorge Sampaoli ikithibitika
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment