ENTERTAINMENT Jin la Izzo B limetumika kutapeli.by j.twiceee
Izzo B, rapper toka Mbeya.. ishu ni kwamba kuna jamaa mmoja kutoka Mbeya anadai kutapeliwa Shilingi elfu 50 na Izzo Bizness kwa madai alituma pesa ili atumiwe T-shirt lakini hakutumiwa.
Izzo baada ya kupata malalamiko hayo… Izzo amesema mara nyingi amekutana na malalamiko kutoka kwa watu mbalimbali kuhusu kutapeliwa fedha na mtu anayejiita jina lake.. wengine anawadanganya kwamba anauza T-shirt zenye jina lake, wengine anawaomba kabisa hela !!
Izzo B ameomba radhi kwa watu waliokumbwa na usumbufu wa jamaa huyo huku akiwaomba kuacha kusikiliza ama kutuma pesa zao kwa mtu ambae hawana uhakika naye na wajue kuwa mtu huyo si Izzo.
No comments:
Post a Comment