Tuesday, June 30, 2015

 Hizi ndio sababu za Facebook kuamua kufungua office zao South Africa.. by j.twice


Nimeipata hii takwimu ambayo sikuwa nafahamu, kumbe Facebook ina watumiaji Milioni 120 wa Mtandao huo ndani ya Africa pekeyake !!

Story nyingine kuhusu Facebook kwa sasa hivi ni ishu ya kusogeza Office zao mpaka ndani ya Jiji la Johannesburg Afrika Kusini na tayari hapo ndio yatakuwa Makao Makuu ya shughuli zao zote zinazohusu Facebook Afrika, Nunu Ntshingila ndio Boss ambaye kachukua ajira kusimamia Kampuni hiyo


Mark Zuckerberg, Boss wa Facebook

Kingine ni kwamba jamaa wameamua kuisogeza Facebook ndani ya Afrika kama njia ya kusogea karibu ya wateja wao wengi ambao ni Wafanyabiashara wanaotumia Mtandao huo katika kutangaza biashara zao.



Facebook iliangalia siku nyingi sana jinsi ya kuingia kwenye soko la Afrika, waliwahi kurahisisha huduma kwa watumiaji wa mtandao huo kwa kuweka App maalum ambayo mtumiaji hakatwi pesa wala hatumii data kwenye kuchat, mpango wao mwingine ni kuhakikisha wanamfikia kila mtu hata ambae hana uwezo wa kumiliki simu yenye uwezo wa Internet.


Nunu Ntshingila, Boss wa Facebook Afrika.

Mpango walionao kwa sasa ni kuajiri wafanyakazi 25 ili ofisi ya Johannesburg ijitosheleze na kazi iendelee kama kawaida.

No comments:

Post a Comment