Breaking News: Taarifa za magaidi Morogoro na picha za walivyokamatwa navyo. By j.twice
Kulikuwa na mfululizo wa uvamizi wa Vituo vya Polisi, watu wakapata hofu wengine walihusisha matukio hayo na ishu ya ugaidi baadae hali ikawa sawa.
Matukio hayajaisha, nimeipokea ripoti ya ITV kutoka Morogoro inayohusu watu watatu kufariki katika mapambano na Polisi, huku wawili kati yao wakihisiwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la Al Shabaab.
Breaking News nyingine kuhusu tukio hilihili iliyoripotiwa na Gazeti la Mwananchi inahusu watu sita kukamatwa na wengine 50 wanatafutwa, walikutwa wakiwa na sare za majeshi pamoja na silaha kama majambia kwenye msitu Mvomero.
Kwenye taarifa iliyofatia kutoka Mwananchi, imesema Mkulima Cassian Peter amefariki mchana wa June 27 2015 kwenye Hospitali ya Bwagala ambapo Polisi mmoja amelazwa na hii ni baada ya kujeruhiwa na hao watuhumiwa wa Ugaidi kabla hawajakamatwa.


No comments:
Post a Comment