Thursday, June 18, 2015

BIBI CHEKA ANATAKA KUOLEWA!!!!!! KAZI KWENUU


Created by j.twice
Kama wewe ni mwanaume na unahitaji mke nafasi hii hapa! ..…Msanii mkongwe nchini Bibi Cheka ameweka wazi kwamba endapo atatokea mwanaume wakapendana kwa dhati yupo tayari kuolewa!

Akichezesha taya zake na mtangazaji ambaye pengine ndio mkali zaidi wa matukio nchini, Mkisi Jr, ambaye anakimbiza na show kali ya Hatua Tatu, Habari Ndio Hii kwenye radio ya Times Fm waliongea mengi huko Bunju B jijini Dar es salaam, Bi. Cheka alisema yeye kama mwanamke anasifa na vigezo vyote vya kuwa na mume wa mtu.

“Nimewahi kuolewa na nilibarikiwa kuzaa watoto tisa lakini baadae tuliachana na mume wangu kutokana na ulevi,” anasimulia Bibi Cheka.

Bibi Cheka aliendelea kusema kwamba, tangu hapo hajaolewa tena lakini kwa sasa kama atatokea mtu wa kumuoa yupo tayari ingawa alipoulizwa kuhusu umri wake bibi huyo alisema hakumbuki mwaka aliozaliwa wala miaka yake!

No comments:

Post a Comment