Saturday, June 20, 2015

BARAKA DA PRINCE KUTOA NGOMA NA PATORANKING WA NIGERIA BY J.TWICE
Mwanamuziki bora Chipukizi anayeibukia kwenye game ya Bongo Flava Baraka Da Prince ambaye anatesa na ngoma yake Siachani Nawe amesema, lengo lake kwa sasa ni kuvuka anga la kimataifa.

Baraka kijana toka jiji lenye mawe mengi Mwanza, alifunguka mengi pale alipokutana na mwandishi wetu, huku akiwashukuru wadau na mashabiki wake kwa kumfanya aweze kuibuka na tuzo ya Mwanamuziki bora Chipukizi anayechipukia, kwenye tuzo za muziki za kilimanjaro kwa mwaka 2014/2015.

“Hii tuzo inanifanya nijiamini zaidi kwenye safari yangu ya kiinternational, na baada ya mwezi mtukufu kuna ngoma moja itatoka ambayo ni tofauti kabisa na nimemshirikisha mwanamke hatari sana itakua ni surprise kubwa”, alisema Baraka.

Baraka aliweka wazi kuwa kimataifa ataanza kutoa ngoma na mkali toka nchini Nigeria Patoranking ambaye anatesa na ngoma yake ya Girlie.

“Tukitoka Nigeria, watu wakae sawa kwani tunamalizia mazungumzo na Jaguar wa nchini Kenya ili tutoe ngoma nyingine kali”, alimalizia Baraka Da Prince.

No comments:

Post a Comment