Diamond Platnumz kwenye kollabo nyingine na msanii Donald kutoka South Africa!! By j.twice
Diamond Platnumz ameendelea kufungua milango mingine ya collabo na mastaa wengine Africa.
Tumehesabu siku siku chache zimezopita toka ilipoachiwa brand new collabo ya Love Boat ambayo Diamond kashirikishwa na msanii wa Nigeria, Kcee.
Kasi ya Diamond haijaishia hapo kwani sasa hivi ameingia tena studio South Africa na msanii Donald kutengeneza ngoma nyingine kupitia Universal Music Studios nchini South Africa, na hapa nina baadhi ya picha za wasanii hawa wawili wakiwa studio wanarekodi nyimbo yao mpya..
Wasanii hawa leo watasikika live kupitia Metro Fm jijini South Africa na badaae kufanya mkutano na Universal Music Studios.



No comments:
Post a Comment