Monday, June 15, 2015

 show ya mwisho kabla New Maisha Club haijahamishwa rasmi Masaki, by j.twiceTZA
onJune 15, 2015


Jana pale New Maisha Club Masaki kulikuwa na party ya kufungwa kwa club hiyo…  Watu wa nguvu walienjoy na burudani ya show toka kwa Shetta, Amini, Dudubaya, Snura pamoja na Nuh Mziwanda.

HK ambae ndio Manager wa Club Maisha amesema wanafunga ili kubadili mazingira, Club hiyo itahamishiwa maeneo ya Kijitonyama nyuma ya jengo la Millenium Tower  ambapo Club hiyo itakuwa kwenye Jengo la underground kabisa.

Utaratibu wa kuhama na kukarabati Club hiyo utafanyika ndani ya kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.. pata picha hiyo Maisha Club underground itakuwaje yani !!

Matukio haya kwenye pichaz yote nimekusogezea kutoka kwenye show hiyo ya mwisho iliyofanyika jana June 14 2015 #Maisha_Club

No comments:

Post a Comment