NEYMAR SHUJAA BRAZIL IKIITANDIKA 2-1 PERU COPA AMERICA, COLOMBIA YAPIGWA 1-0
TIMU ya taifa ya Brazil imeifunga mabao 2-1 Peru katika mchezo wa Kundi C michuano ya Copa America usiku wa kuamkia leo nchini Chile.
Christian Cueva alitumia makosa ya beki David Luiz kuifungia Peru bao la kwanza dakika ya tat utu ya mchezo, kabla ya Neymar kuisawazishia Brazil dakika ya tano.
Bao hilo linamfanya Neymar aweke rekodi ya mchezaji mdogo zaidi kufikisha mabao 44 katika timu ya taifa ya Brazil, akivunja rekodi ya Pele.
Mshambuliaji wa Liverpool, Philippe Coutinho aliumia na ataukosa mchezo ujao dhidi ya Colombia.
Neymar akamsetia Douglas Costa kuifungia bao la ushindi Brazil dakika ya 93. Mchezo mwingine wa kundi hilo uliotangulia, Venezuela iliifunga 1-0 Colombia
Kikosi cha Brazil kilikuwa: Jefferson, Alvez, Miranda, Luiz, Luis, Fernandinho, Elias, Willian, Fred, Diego Tardelli na Neymar.
Peru: Gallese, Advincula, Zambrano, Ascues, Vargas, Ballon, Lobaton, Sanchez, Cueva, Guerrero na Farfan.
No comments:
Post a Comment